UKUMBUSHO
PDF
Mhubiri 12:1-7.
1 Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo;
2 Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua -------------- Nayo mavumbi kuirudi nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
KUMBUKA ULIVYO SIKIA.
Roho wa Aishiye kila wakati analifikia Kanisa ili kuleta ukumbusho wa yale mambo lililopokea kutoka kwa Baba na utukufu wa hilo Kanisa uko mkononi wa kuume wake Mungu. Twayaona haya katika muktadha wa ile tarumbeta ya kwanza na ya tano ambazo zalingana na jumbe kwa makanisa yaliyo Sardi na Efeso katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana.
Ufunuo 3:3 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyokosea; yashike hayo na kutubu
Ufunuo 2:5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza;
Ukumbusho wa vitu tuliyosikia na kupata kutoka kwa Baba ndiyo hurejesha na kuliweka kanisa katika utukufu wa Bwana kwa milele yote. Kila wakati binadamu anaposahau nong'onezo la utulivu kutoka kwa Roho na anajifunganisha na uongo utokao vilindi vya kuzimu, anapoteza ujuzi wake wote kujihusu na kumhusu Baba. Ule ukumbusho unapoisha, yule mwanadamu huponyoka kutoka vilele vya utukufu na kuingilia giza totoro na kifo, milki ambayo wanaomsahau Bwana huishi (yaitwa ‘ulimwengu’). Mwandishi Zaburi akiri haya anaposema na kuandika, …Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. [Zaburi 6:5, Zaburi 9:17, Zaburi 88:11-12].
Amin, amin, Kile ulichonenea gizani kitasikika kwenye nuru; na kile kilichonenwa sikioni kwenye maficho kitatangazwa juu ya dari.
Unaporejelea kile ulichonena na kusikia kwenye giza katika nuru ya kweli ya Roho, kupitia utulivu na tafakari, unaanza kutizama na kuona Ufalme ulio wa Kweli hewani (rohoni) ukifunuliwa. Pamoja na mbingu hizi mpya na nchi mpya, kwaja kutokomea kabisa kwa husiano zote za kilimwengu na sisi twaridhi hiyo hiyo nchi mara mia katika Ufalme wake Mungu, ulimwengu haswa usioharibika tena kamwe.
Mathayo 19:29 Na kila mtu aliyeiacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.
Ni kama kipepeo anavyochipuka kutoka ndani mwake yeye mwenyewe. Vivyo hivyo ndivyo mwanadamu katika tafakari anavyoanza kuangalia ndani na kuvumbua mtu tofauti wa kiungu, na ulimwengu mpya. Huyu mwanadamu lazima asake na asikome kutafuta hadi apate kuvumbua tena mtu wa kimbingu aishie ndani mwake. Kwa tafakari, lazima akawezepenya kulivunja shehena la mtu wa nje na akaweze kutafuta tena mabawa yake ya kimalaika, na vazi lake la rangi nyingi, mabawa ambayo kuyapitia hayo ataweza tena kupaa katika mbingu na kuyafikia maji matamu ya mito ya Uzima.
KUINGIA PALIPO TULIVU
Kwa kuisikia sauti ya Kweli, ukumbusho na kutiwa nuru huja katika mioyo ya wanadamu. Kwa kunyamaa na kutulia kwenye tafakari na maombi huleta ukumbusho wa Kristo ndani, ambaye ndiye mfano wa Mungu asiye uharibifu na asiyeonekana. Wengi wetu wamesikia mambo mengi na makuu kwa muda mrefu sasa, bila kitu cha kuonyesha kwa kile walichosikia. Kwa ajili ya hili itabidi tuanze kukumbuka tulivyopokea kutoka kwake Baba na tujikaze katika yale kwa nia moja. Huyo mwanadamu ataridhi Baraka zisizo kipimo kutoka kwa Mungu wake, asiposikia tu. Itambidi aingie kwenye ule utulivu na kunyamaa, mbali na kelele zisizopimika za Babuloni na mbali na nyuso za wanadamu walio chini yake na akaanze kusikiza tena zaidi na kufanya kazi zile za kwanza tangu Mwanzo, alipoona uso wa Baba pekee.Hili huletauamsho na ukumbusho wa ule utukufu wake Mungu ulioko ndani mwetu.
Kama ile mifano viashiria ya Yesu, Eliya, Musa na wana wa Israeli, mwanadamu lazima aenende katika zile siku (au miaka) arobaini ya kujitenga katika ile safari ya kiroho ndani ya moyo wake Mungu mahali ambamo atasikia tena na kuungamanika na ile sauti tulivu ya Yule Aliye Milele inaposema MIMI NDIYE, na kando yangu hamna Mungu mwingine, kwa sababu Mimi Ndiye nimilikiye Milele yote. Ni ile hali ya kupenya kupita zile pazia za kiza la maisha ya wanadamu kwa kukumbuka na kujua kwamba Kristo aliye Mungu Kweli na Uzima wa Milele Ndiye Uhai wetu. Ukumbusho huu ambao ni katika utulivu na tafakari humwamsha mwanadamu kwa ukweli kuwa mimi ni Mungu, kwa sababu huu ndio Uhai wetu; haya maarifa humkweza mwanadamu juu ya mambo ya ukafiri ulioko chini yake. Na kama mwanadamu hajui siri takatifu ya MIMI NDIYE, yeye hukusanywa katikati ya makafiri wasiomjua Mungu.
Zaburi 46:10 Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitatukuzwa katika mataifa, nitatukuzwa katika nchi.
Lile jangwa linalohusishwa na zile siku arobaini (au miaka arobaini) zazungumza kuhusu kujaribiwa na majaribu yanayoambatanishwa na sauti zipingazo za kutoamini ambazo hufanya kazi kupitia nia ya kimwili ili kumfanya mwanadamu ashushike moyo anapopaa kuingia katika Ukamilifu wa Kristo. Hizi sauti za kutoamini hutafuta kukufanya uurudilie ule usingizi wa kiwiliwili cha kuwa wewe ni mtu wa kawaida. Zile sauti hukufanya uache ile safari na kusongelea raha za kilimwengu na kubaki umefunganishwa katika zile sauti za Babuloni iliyo chini. Lakini twahitaji kujua kuwa hii safari sio ya waliodhaifu, mbali ni ya wale walio ndani yake kuimaliza ile safari liwe liwalo.
Katika safari yake, hata Elijah mwenyewe alisongwa na usingizi, mpaka wakati alipogutushwa na kutiwa nguvu kutoka juu.
1 Wafalme 19:5 Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazamu, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. 6 Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena. 7 Malaika wa Bwana akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako. 8 Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
Bwana yu hapa kutupa nguvu tena;lazima tuendelee katika ushirika na neno na kupokea nguvu kila wakati na kuongeza ujuzi katika mtu wa ndani, kwa kusherehekea chakula kile wa malaika. Bwana katika uaminifu wake hawezikubali tukose neno kutoka mbinguni. Mungu awezavuvia roho zetu kwa neno lake ama pia awatume watumishi wake kuleta lile neno. Kupitia nguvu za huu mkate (Neno la Kweli), kama Eliya, lazima kupae kiroho mpaka tujijue kwa uhakika kuwa tu kilele cha Mlimani Horebu (ishara ya Sayuni), mahali ambapo sauti tulivu yake Roho yasikika kwa uhakika.
Kama una ushahidi moyoni kwako kuwa sauti yake Baba yakuita upande hata huku, usishushwe na pingamizi zilizoko ndani na nje. Kumbuka kuwa wewe u vile ulivyo mbele ya uso wake Baba na hakuna kilicho cha mwili kinawezabadilisha hicho. Mwache Roho akuongoze wewe hadi kilele cha Sayuni mahali ambapo utaingia tena kwenye ushirika na Sauti yake Baba. Kileleni mwa Sayuni wewe utatambua mwili wako wa nuru kama ule ule uliokuwa naye Yesu alipofunuliwa mlimani. Huu mwili waashiria hali ya mwanadamu anapofufuliwa toka kwa wafu.
Uwezo wake Eliya naye Musa kusikia na kushiriki na sauti hii tulivu lakini ngurumo pia ndio iliyowafanya wao kuwezapotelea nguvu za kaburi humo chini.
Baada yake Eliya kuisikia sauti hii mlimani Horebu, Eliya alitwaaliwa kupitia upepo wa kisulisuli kati ya gari la moto na waendeshaji farsi wa moto, ambalo ni mfano na ishara ya kubadilishwa kutoka mtu wa kilimwengu hadi kuwa mtu wa Roho ambaye kama tujuavyo ndiye Bwana kutoka Mbinguni [2Wafalme 2:11]. Nao huu ndio mwisho wa imani kwa wale ambao wanawezasikia na kuungamanika na Kweli. Kusikia sauti ya Roho kwa ukamili, humwamsha mwanadamu na kumkumbusha yeye kuwahusu wale waendeshaji farasi wa moto na kuwa yeye kwa kweli ni (Roho). Kwa ukumbusho ule, yeye hukwezwa toka duniani – kutoka kwenye kiwiliwili cha uhai wake wa kiwanadamu na kwa mara nyingine hukusanyika na ndugu wenzake wa kimbingu wanaowakilishwa na mamilioni ya malaika na magari yaliyokusanyika katika Jina la Bwana mlimani Sayuni kwenye kilele cha viumbe vyote [Zaburi 68:17, Waebrania 12:22-23].
Huu mpango wa kutukuzwa ambao mara kwa mara twasikia; kutukuzwa na kukumbushwa kwaambatana moja kwa moja.
Zaburi 104:3 Na kuziweka nguzo za orofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, Na kwenda juu ya mabawa ya upepo, 4 Huwafanya malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa moto wa miali.
Kutukuzwa kwa malaika wake Mungu (watumishi wake) na watumishi katika mawingu, upepo, roho na miale ya moto kwaletwa na ukumbusho unaoletwa na kusikia Sauti Yake Roho. Kutukuzwa kwao watakatifu kunaambatana na kukumbuka na kuvumbua tena hali yao ya kiungu ambayo walipoteza katika usingizi wao wa kifo. Walio wafu katika kaburi la kusahau kwa uwanadamu wao wasikia ile sauti ya Kweli na katika vitanda vyao vya kuzimu wanaanza kukumbuka tena hali zao za kiungu. Wanapokumbuka mambo yaliosahaulika, kama Lazaro, wanapaa toka kenye mavazi ya makaburini na kufunguliwa pingu zilizowafungunisha na nira kuu katika uasi wa siku tulizoko za upumbavu.
TUTIZAME KUPAA KWAKE MUSA.
Tukimwangalia Musa, mwili wake haukupatikana ilhali alionekana pamoja naye Eliya wakati Yesu alipotukuzwa mbele yao wanafunzi wake. Hili lapaswa kukupa jambo la kutafakari. Mtu awezasema kuwa Mungu ndiye aliyemzika Musa. Lakini itakubidi usikize Roho wala sio maandashi kutoka kwenye kitabu kiitwacho biblia. Lazima tutambue kuwa Mungu sio Mzika Wafu, kumaanisha kuwa yeye hako kwenye biashara ya kuwazika wafu; yeye ako kwenye kazi ya kuwafufua waliokufa na kuwahifadhi walio hai katika uhai huo. Mungu hana mkataba wowote na walio wafu.
Wacha niwape jambo linguine la tafakari. Wakati yule malaika mkuu alipovutana na Shetani kuhusu mwili wa Musa, ilikuwa wauzike au wauvuvie? [Yuda 1:9].
Wakati mwingine wowote ambao malaika mkuu anapotajwa katika biblia ni wakati anapowasaidia watakatifu katika ufufuo wa wafu. Katika 1 Wathesalonike 4:16. Analeta ukumbusho na uamsho ndani ya watakatifu kwa Kupigwa kwa Barangumu (Kelele) Ambayo yaashiria sauti ya Kweli inayotiririka kutoka Moyoni wake Baba. Katika huu uamsho, wao tena wakusanyika katikati ya umati wa watumishi na mashahidi (yale mawingu) – wakusanyika hewani (Rohoni) katika jina la Bwana.
1Wathesalonike 4:16 Kwa sababu Bwana Mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza: 17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
Malaika Mkuu Mikaeli anatajwa tena katika kitabu cha Danieli anaposimama kuwasaidia watakatifu katika ufufuo wa wafu, wakati wale waliolala kwenye mavumbi, katika ubatili wa uwanadamu. Hawa ni wale wanaovumbua tena Nuru yao ya kiungu katika mfano wa Mungu Aishie na wanaingia uzimani.
Danieli 12:1 Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu mfano wake hautakuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. 2 Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. 3 Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.
Tokana na haya yote twaona kuwa malaika huyu mkuu katika uhusiano wake na mwili wake Musa, inalingana na kuwavuvia na kuwafufua wafu tuko mavumbini. Kukinena kwa viashirio, Roho aonyesha kuwa Musa alipaa kuingia katika lile kusanyiko la kiungu la roho zilizokamilika, kama vile Eliya alivyofanya. Hata kama haijulikani kwa wengi, ni Kile Kiumbe cha kimalaika kilichomsaidia Eliya jangwani [1 Wafalme 19:5-7], na akamtia Yesu nguvu alipoelekea msalabani [Luka 22:43]. Kumbuka, ni ule ufunuo Roho anaopeana unaohitajika, kwa hivyo haihitajiki wewe kujaribu kutambua hili kwa akili za kiwanadamu.
Inatubidi tujiulize, ni nini kilichomhitimisha Musa kuingia katika hatima hii tukufu? Kwa kuashiria, huo mkutano aliokuwa nao na lile tawi lisiloungua pale kileleni mwa mlima Horebu (mfano wa Sayuni), Musa alitembea katika upya wa uzima katika nguvu za ufufuo. [Kutoka 3]. Alikuwa ni mtu mpya aliyetembea katika jina mpya, jina la MIMI NDIYE. Alipotokea usoni mwake Mfalme Farao, ilikuwa ni ashirio la Mungu Mkuu anapotokea katika utukufu mkuu na nguvu katika mwili kuwakomboa walioteuliwa kutoka kwa nguvu zake Yule Muovu. Hii ndio siri ya uungu inayonenwa naye mtume Paulo katika waraka wake kwa mwanawe Timotheo:
1Timotheo 3:16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulikana kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Kile Waisraeli walichokiona, wakati Musa aliyetukuzwa alipotokeza mbele zake Mfalme Farao na Misri yote, ni ishara ndogo tu kumhusu Mungu asiyeonekana anapodhihirika; waliuona utukufu wake Mungu Mfalme ambao ulikuweko pale Mwanzo, ambaye Kwaye vitu vyote viliumbika na ndani Yake vinashikamana.
Baada ya kuisikia sauti ya ndani ya Kweli inayofunua ukweli wa MIMI NDIYE, Yule mwanadamu wa kale wa mwili na nyama anayeyuka, ili abakiye awe ni Bwana wa Mbingu pekee. Musa aliyefanyika upya anaashiria wana wa ufunuo wasiokufa; hawa wameamka kuingia katika ukweli wa Aliye Mkuu ndani mwao, Ambaye Ndiye Umbo na Mfano Mungu asiyeonekana na asiye uharibifu.Hawa wakuu wameshinda kiwiliwili cha maisha ya kiwanadamu kilichoko humu duniani na wamevumbua tena kupitia kutiwa ule ukumbusho kuwa,
MIMI NDIYE BWANA, NA KANDO YANGU HAMNA MWINGINE.
Bwana alimpa Musa ishara ambayo indumu kama ishara ya milele kwake kila mtu atakayeivumbua ile hali ya Uzima ulioko katika Roho wa Milele. [Kutoka 4:3-4].
Marko 16:18 …watashika nyoka…
Mungu alimwambia Musa aachilie fimbo yake iliyokuwa mkononi mwake, iliyogeuka na kuwa joka kuu hadi Musa mwenyewe akalikwepa, kuonyesha kweli kuwa lilikuwa joka la kuogofya. Baada ya hili, Mungu alimwambia Musa aliokote tena kwa mkia wake na likageuka tena na kuwa fimbo yake kama mwanzo. Hili laashiria vile, katika kushuka kwake kuingia katika uwanadamu, mwanadamu alipoteza milki yake na hitimisho lake la kiungu na akawa kitu dhaifu na kinyonge, na kinacho tabia na miigo ya lile Joka (Yule mnyama) ambamo mwatoka ile sumu isiyoisha (dhambi na uasi). Lakini wakati mwanadamu anpoanza kusaka na kusikia tena kama Musa alivyosikia kwa miaka arobaini, yeye atashinda unyonge na uharibifu wa Yule mwanadamu-joka aliye wa mavumbi na akawezevumbua tena milki yake aliyopoteza. Huu ndio ule wokovu umngojao yeyote Yule asikiaye ukweli na kutenda katika ile kweli. Huu pia ndio ushindi dhidi ya hali zote zile za Yule mnyama tumwonaye katika kitabu cha Ufunuo.
Ufunuo 15:2 Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa Yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu. 3 Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, nay a ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa. 4 Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.
Yote ni kuhusu kukumbuka katika utulivu; ukumbusho hufufua mwanadamu kuingia katika ukweli kuwa yeye ni umbo na mfano kabisa wa Mungu, asiye uharibifu, wa milele, asiye mwili, na mkamilifu. Katika uvumbuzi huu wa kiungu, kile kinubi na zeze lililo ndani chamwamsha mwanadamu, anapoimba wimbo wake Mungu Mkuu, kwa ajili wa uimarifu na ukuu wake uliokuwa umefichika, sasa umefunuliwa.
Zaburi 57:8 Amka, utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri.
MKUMBUKE MUNGU BWANA WAKO SIKU ZA UJANA WAKO
Siku za ujana wetu ndizo siku ambazo mwanadamu hutembea katika utimilifu wa Utukufu wake Mungu, anapoutambua Uhai wa Kristo usio mawaa na usio na mwisho wake. Mtume Paulo asema kuwa Kristo ndiye Uhai wetu; ikimaanisha kuwa Uhai wake Kristo aliyefunuliwa pale mlimani ambao haujui wala kutambua kuangamizwa naye Mungu, uoga, ugonjwa, uchungu, huzuni, uharibifu nk. Ndio Uhai wetu Huu Uhai usio mawaa ndio Uhai halali wake mwanadamu bila kikwazo chochote kuambatana; kukumbuka kwake huu Uhai tu ndiko kumfanyako yeye kuikumbuka hii siri.
Wakati Yesu aliumega ule mkate wa ushirika na ile divai na wafuasi wake kwenye lile jumba la juu, lililoashiria Mbingu, Alikiri kuwa ule mkate ni Mwili wake, na ile divai, Damu yake. Alionyesha kuwa sisi ni Mmoja katika Roho na kuwa sisi sote ni washirika katika ule Uhai Mooja, Mwili Mmoja, kwa kuwa uhai wa mwili u damuni. [Mambo ya Walawii 17:11-14]. Alipoyafanya haya, Aliwaamurisha wafanye lile katika ukumbusho wake. [Luka 22:19 -20]. Hili jambo lina maana ya undani zaidi kushinda kushiriki mkate tu wa kawaida katika tamaduni za kushiriki Meza Ya Bwana inayofanywa na wanadamu. Hilo jambo Yesu Alilolifanya katika ile karamu ya jioni ni fumbo likiashiria Ushirika wa Kimbingu ndani mwake Kristo. Inaashiria Ushirika wa Uzima uliofichika ndani ya Mungu ambao kila mwanadamu ni lazima aushiriki ili apate kuishi; awaye yeyote aliye nje ya Ushirika huu wa Mbingu ni mfu.
Yesu kwa hiyo akawaamurisha wafuasi wake kulifanya lile katika ukumbusho wake.Ni nani na ni nini tunachokikumbuka hapa? Je, ni Yesu wa kijinsia ambaye alizaliwa na bikira Mariamu na akafanyika basi wa ukoo wake Ibrahimu kulingana na mwili? Kama Yesu mwenyewe alinena kujihusu, kulingana na mwili, haingewezekana kwake kusema: yeye Ibrahimu asijakuwako, MIMI NIKO.(Yohana 8:58).Wala hangewakana mamake mzazi na nduguze hadharani, akikiri kwamba, mamake wa kweli na nduguze ni wale wasimamao naye katika Nuru wakiyatenda mapenzi yake Mungu.
Akawajibu, akisema, Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani? Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akasema, Tazama, mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana mtu yeyote atakayeyafanya mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu. (Marko 3:33-35)
Yesu Kristo ni Ishara ya Uzima na ni Mfano wa Mungu Aishiye, Mungu Aishiye katika Mwili, kupitia Kwake Yeye Ambaye vitu vyote vilivyomo, vinavyoonekana na visivyoonekana viliumbika. Yeye Ndiye Alfa na Omega, Mungu mwenye Nguvu, Yeye Aliye, Aliyekuweko, na Atakayekuja. Hii yazungumzia hali halali naya ukweli, isiyo nyonge, ya Kiroho, ambayo si mwanadamu wa kijinsia, hata ingawa yawezatokeza kama mwanadamu, kama vile Yesu Alivyotokeza na Anatokeza kupitia sisi ambao wameamka muda na wakati huu. Kama Kanisa, Mwili wake Kristo, kazi yake Roho ni kutukumbusha kuwa sisi sote ni washirika katika huo Mwili usio na unyonge, usio na mwanzo wala mwisho.
1Yohana 5:20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.
Kuendelea katika huu ufunuo utokao juu kwaleta ukumbusho na kwamhifadhi mwanadamu katika Nuru kama vile Yeye Kristo ni Nuru, mbali zaidi na milki ya kimwili mahali ambapo uharibifu watamalaki bila pingamizi lolote lile. Wakati mwanadamu atembea katika huu ufunuo, mambo yote yawezekana na anapata kitu chochote kile anachohitaji, kwa sababu nguvu kuu za Mungu mwenye Nguvu zatiririka kumpitia yeye kwa imani. Huu ndio ukumbusho ambao kila mwanadamu aitwa akaweze kuishi ndani mwake. [Mhubiri 12]
Mhubiri 12:1-7
1 Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku zilizo mbaya…………………..
Tumedhibitisha kuwa mambo yote yalifanyika kupitia Kristo, Ambaye kwa uhakika, ni Mungu anayejidhihirisha kama mwanadamu. Tumedhibitisha pia kuwa sisi sote ni washirika katika lile kusanyiko liitwalo Kanisa, ambalo ni Mwili wake Kristo. Tupate hili dhahiri; kichwa bila mwili hakina maana. Cha kushangaza sana zaidi ya yote ni kuwa sisi ni mmoja katika huu Mwili wa Kiroho na wa Kimbingu, kupitia kwao vitu vyote viliumbika na vyahifadhika. Sisi tulikuwa katika huu Ushirika wa Kiungu kabla huu ulimwengu kuweko. Mambo kama haya husikika ni kama ya kijuha na yasiyoeleweka kwake mwanadamu wa kawaida, kwa sababu ameteleza na kuanguka katika shimo kuu la kiga la kusahau.
Katika kiza la kusahau linaoitwa dunia, binadamu huanza kusongwa na maovu ya siku anazoishi, ambapo furaha ya Paradiso huisha na mwanadamu huingia katika hali mpya ya kuhisi uoga na kusaga meno. Nuru ya mbingu na sayare na nyota hata mvua toka mawinguni huisha, kumaanisha kuwa mwanadamu hushuka kutoka ile hali ya Kimbingu na Ushirika katika Nuru (ambalo ndilo Kanisa). Mwanadamu huanza kutembea tena kama kiumbe kilichotiwa nira katika mambo duni ya kijinsia ya kilimwengu, wanapopoteza ufahamu wote wa kuwa yeye ametoka kwake Muumba. Mambo yake huanza kusambaratika na kupasuka msamba anapofanyika kijakazi kwa nguvu hizi za uharibifu za kiza.
Mhubiri 12:3-6 anakili hali ya uharibifu inayozidi kudhoofika ya mwanadamu anaposongwa na siku hizi ovu mahali ambapo kifo chatawala bila pingamizi.
Ecclesiastes 12:3-6 Siku ile walinzi wa nyumba watakapotetemeka (mikono); Hapo wenye nguvu watakapojiinamisha (miguu); Na wasagao kukoma kwa kuwa ni haba (meno); Na hao wachunguliao madirishani kutiwa giza (macho); Na milango kufungwa katika njia kuu; Sauti ya kinu itakapokuwa ndogo (kazi zadidimia); Na mtu kusituka kwa sauti ya ndege; Nao binti za kuimba watapunguzwa (hamna tena kuimba na furaha);----------------
Ni kuteleza kusikoisha kuelekea katika uharibifu kwa sababu yeye ni mpumbavu na haelewi kuwa Bwana ndiye Uzima na Uhai wake wa kweli. Ndani ya hili ndiyo sababu uharibifu na tama za mwili zatia uchafu ulimwengu mzima huu tulio; ndio maana wengine ni wagonjwa, wengine ni wanyonge katika imani kwa sababu katika hali yao ya kifo, hawawezi kuutambua Mwili wake Bwana ambao wao no mmoja katika Huo.
Na tuweze kutafakari waraka wake Paulo kuuhusu huu Mwili wa Bwana:
1Wakorintho 11:24-30 naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mlapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili. Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala.
Mahali hapa, huu Ushirika wa Meza ya Bwana umekuweko daima kuanzia misingi ya Dunia. Wanadamu huhisi maovu wanayoyahisi kwa sababu wao hufanyika wasiostahili Utukufu wake Bwana. Wanadamu walianza kushiriki meza za kishetani (‘kishetani’ kikiwa ni ile hali ya ‘mwanadamu-jinsia’) na wakapoteza hali yao yote ya kutambua ukweli wa Mwili wa Bwana ambao wote ni mmoja nao.
1Wakorintho 10:21 Hamwezi kushirikiana meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.
Hili ndilo lililofanyika wakati Adamu, ambaye alitembea katika Utukufu wa Ile Nyota ya Asubuhi, akaanza kuwa na ushirika na lile Joka ambalo laashiria hekima ya kimwili ya ulimwengu huu tulio. Ushirika wa aina hii huwafanya wanadamu kuwa na mapenzi kimahaba na sanamu, vitu ambavyo sio Mungu mbali ni wanadamu. Hakuna yeyote anayewezaungamanika na ashiriki katika Meza ya Bwana na aweze tena kushiriki katika meza ya kishetani; huweziishi katika ulimwengu wake Mungu na wa kishetani.
Katika kufunuliwa kwake, Yesu Amekuja kurejesha huu ushirika ambao kwa mara nyingine waleta ukumbusho wa Mwili wake Bwana Ambao sisi wote ni mshirika. Tunapomkumbuka Bwana katika Ushirika huu kimaombi, Yeye huja ndani mwetu, kwa sababu sisi ni Yeye, na Yeye ni sisi. Tunatambua tena urembo ulioko katika Uzima usioisha wa Upendo, na kutendeka kwa mambo kusikoisha.
Kumbuka kuwa Aliye Mkuu ndani mwetu, hugeuza hali ya kifo na humfanya mwanadamu kuvumbua tena nguvu za ujana wake; hii hali humrejeshea yeye zile siku za ujana wake wakati hakukua na vikwazo vyovyote. Inahusu kutambua Kristo Aliye ndani mwetu, Yeye Aliye jana, leo, na milele. Mwanadamu akiwezapokea mafunzo kutoka kwa Roho ambayo yanaleta ukumbusho, yeye atakwea kutoka kwenye shimo la kusahau, mahali ambapo uharibifu watawala na mara tena akazione siku za ujana wake; Yeye atatambua umaridadi na urembo wa vile yeye alivyo. Huu ndio wokovu wake Bwana.
Ayubu 33:23-26Kwamba akiwepo malaika pamoja naye, Mkalimani, mmoja katika elfu, Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo; Ndipo amwoneapo rehema, na kusema, Mwokoe asishuke shimoni; Mimi nimeuona ukombozi. Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya motto; Huzirudia siku za ujana wake; Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia; Hata auone uso wake kwa furaha; Naye humrejezea haki yake.
Twawezamalizia kwa kusema kuwa ukumbusho ni kitendo cha kuabudu; ni kutizama, na kuomba, na kufunga; ni uwakilishi wetu ambao humfanya mwanadamu kuupotelea uharibifu wa jehanamu humu chini na kumhifadhi yeye katika Uzima milele yote. Wanadamu wote ni lazima wasimame wima katika ukumbusho na watambue ya kuwa BWANA NDIYE UZIMA WANGU. Hii ndio kweli ambayo Roho Awachilia juu yetu sasa; Hili lapoza mioyo yetu iliyochoka kwa kuleta ukumbusho way ale mambo ya Utukufu yaliyosahaulika katika maisha yetu ya kiwanadamu. Mtu akijihisi kuwa ako pweke, ameachwa, amenyenyekezwa, ameumizwa kihisia, mgonjwa, ama lolote lile, tulia, angalia ndani mwako na ukaweze kukumbuka Kristo Aliye ndani yako; Yeye ndiye Lango kuingia katika ulimwengu mpya wenye vinjari, mahali ambamo hamna kikwazacho, wala kitiacho uongo kupenya pale.
Mungu Akubariki.
Trevor Eghagha
trevor@sunrayministry.org
www.sunrayministry.org