WALE 144000 WALIOKO MLIMANI SAYUNI
Ufunuo wa Yohana 14.
1 Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama
juu ya Mlima Sayuni, na watu mia na arobaini nanne elfu
pamoja naye, wenye jia lake na jina la Baba yake
limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. 2 Nami
nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji
mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti
niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi,
wakivipiga vinubi vyao; 3 na kuimba wimbo mpya mbele ya
kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wane, na wale
wazee; wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule,
ila wale mia na arobaini na nne elfu,
walionunuliwakatika nchi. 4 Hawa ndio wasiotiwa unajisi
pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio
wamfuatao Mwana-kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa
katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.
5 Na katika vinywa vyao haukunekana uongo. Maana hawana
mawaa. |
PDF
Macho ya ndani ya Mtume Yohana yalifunguliwa yakaweze kuona
maono ya ajabu yanayofunuliwa machoni pa mataifa hata wakati huu
tuliomo.
Aliupata ufunuo mkuu la kundi tukufu la mia na arobaini na nne
elfu waliokuwemo Mlimani Sayuni. Lakini hili sio kundi tu lenye
hesabu Fulani. Huu ufunuo wa kundi hili ni uashirio wa wale
waliokombolewa na Mungu, na hili ono hufanyika na kuendelea
kufanyika hata milele, ikiwa ni jambo linalofanyika wakati huu
na kuendelea hata vizazi na vizazi. Hili kusanyiko la kimbingu
hufanyika wakati mwanadamu anapojivumbua kutokana na kushikamana
kwa utope wa kuishi kiwanadamu, na kuanza kukwea na kupaa
kurejelea utukufu wake uliohitimishwa kwenye upeo wa Ufalme wa
Mungu.
Kilele cha Mlima Sayuni
– ambacho ni furaha na tumaini la vizazi visivyohesabika, ni ni
upeo wa kiroho ulioinuka na kukwezeka, mahali ambapo Ufalme wa
Mungu – mji wa Milele wa Mungu Aishie, ambo kwa jina jingine
waitwa Jerusalemu ya Kimbingu wapatikana. Klele hiki chaashiria
chanzo na hatima ya kila kiumbe, ambapo kila kilicho hai huwa na
chanzo chake na pia huhifadhika; mahali paishipo Uwepo
usiopimika, Nguvu na Utukufu wa Mungu Aishie.
Hili kusanyiko ling’aalo
Mlimani Sayuni, ni kweli fulani iliyoko hata wakati huu tuishio,
wala sio jambo lijalo wakati fulani wa siku za usoni, vile wengi
wetu wamefanyika kusadiki. Ni hali ilioko ambayo ina utukufu, na
ambayo Mungu anatamani kila mwanadamu akaweze hitimia, Ufalme wa
Amani kamilifu, utangamano na Utukufu. Ulimwengu unapoyumba
mbele na nyuma kwa kukosa uhakika na kujawa na uoga, unapoyumba
kwa ulevi wa uongo wake, kubobea, kunawiri na amani ya mahali
hapa patakatifu pazidi kutotikiswa wala kutetemeshwa milele.
Kila mwanadamu mwenye
roho wa kupambanua mambo na ambaye kwa ujasiri ataisikia sauti
ya Yeye Ambaye Ndiye Mchungaji Pekee wakati huu, atajipata
akitembea katika hali hii iliobarikiwa, kileleni mwa Mlima
Sayuni, kati ya wale Mia na Arobaini na Nne Elfu, waliokombolewa
toka kati ya wanadamu. Sauti iliyo nyororo inayosikika katika
vilindini vya mtu aliyekwepa uzembe rohoni, itamwongoza na
kumshauri kutoka msimu wa kiza hadi msimu wa nuru, mahali ambapo
kifo, kilio na huzuni havimo tena.
Hawa waliokombolewa
wasimama kama nuru ya ulimwengu – wao ndio Yerusalemu Mpya
inayoshuka, kufunua uzuri wake wa kimbingu mbele ya macho ya
ulimwengu wote, kwa utukufu na heshima ya Aliyewaita na kuwatwaa
kutoka kizani kuingia katika Nuru Yake Kuu.
Katika maono haya makuu
ya kimbingu, Roho afunua hali tukufu ya wae ambao watahitimu
kuingia katikahali hii ya ya ukamilifu na ututkufu usio kipimo
ndani ya na kama Mwana ambaye ndiye Kristo.
Mia na Arobaini na Nne elfu
yamaanisha nini? Mia na Arobaini na Nne Elfu (ambayo ni 12 X
12 X 1,000) ni nambari inayoashiria Wana. Israeli
kama taifa liliundika kwa jamii kumi na mbili. Wanafunzi wa Yesu
pia walikuwa kumi na wawili. Inaashiria wana wa Ufalme ambao
wamefikia ukamilifu wa hatima ya kimbingu ya Kristo. Kiroho,
1000 ni nambari inayotumika kuashiria kitu kisicho kipimo.
Lazima tuwe maakini ya kwamba mambo yanayohusu Mungu na Ufalme
Wake, hayawezi nakilika wala hesabik kutumia vipimo vya
kiwanadamu kama wakati na muda, idadi wala kiwango; Mungu
hutumia hivi vipimo kama viashirio na ishara za kudhihirisha
hisia Zake zikilinganishwa na hali Yake ya kutoonekana,
kufichika kwake, na Umilele wa Ufalme Wake.
Wale wajipatao Mlimani
Sayuni, kati ya umati wa waliokombolewa kutokana na kukamatwa na
nguvu za kifo, mauti na uharibifu na wanasimama katika uhuru
mtukufu wa wana wa Mungu, wakiwa huru kutokana na nguvu za
dhambi na dhamiri iliyosongeka. Hawa husimama bila najisi mbele
ya Kiti cha Enzi cha Mungu katika upendo bila chembe yeyote ya
kuhukumika wala dhamiri ya dhambi; wanaishi katika uwepo wa
Utukufu Wake. Hiki ndicho kilele cha kiroho cha uwepo mkuu
Mungu, mahali ambapo Bwana amekuja kuwakusanya watafutao wokovu
wake. Kwa ajili ya hili, Baba kupitia sauti ya Mwana asema:
Nitarejea kuwakusanya, ili NILIPO, nyinyi muwe pia; huu ndio
mwito ulioinuliwa uwaitao wanadamu wawezao kusikia wakiitwa
kushiriki wakati na saa kama sasa.
Kuelewa kwetu
kunapoimarika, na mwanadamu anafanyika zaidi na zaidi
kupsmbsnukiwa na najisi iletayo uharibifu, twahimizwa kuitorokea
ile najisi iletayo uharibifu na kuukwe mlima ulioinuka.
Marko 13
14 Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa,
(asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie
milimani;
Mungu anapeana ishara
hii ya kiroho kwa wapenzi wake walio na masiki ya kusikia kile
Roho asemacho. Chukizo la uharibifu ni umbo la mnyama Yule na
jka lile ambalo ni mtu wa dhambi lisimamalo kwenye mahali pa
Mungu ndani yetu (kwani sisi tu Hekalu ya Mungu) wakati wanadamu
walilala katika kiwiliwili sha kuwa wao ni watu wa jinsia. Yesu
asema kwa wana wanaoweza kuipambanua kweli, kwamba nuru ya
ufunuo wa Kristo inapong’aa, mzifungue nafsi zenu kutokana na
kila hali ya kusongwa na Shetani ambayo imewafunga kwa jela la
utu batili wa kijinsia na ukaweze kupaa Mlima wa kiroho wa
Mungu, uitwao Sayuni. Wale ambao, kwa uvumilivu watamfuata
Mwana-Kondoo katika kizazi hiki kutokana na hali inayokufa ya
mwanadamu wa kijinsia, ambayo wameishikilia kwa muda wa maisha
yao yote, kuingia kwa umbo la kiungu la mwana wa Mungu, ni wale
ambao watajipata Mlimani Sayuni, wakiwa wamenunuliwa kutokana na
wanadamu walio duniani. Kila mwanadamu ameitwa akaweze kuhama
kutoka sehemu za chini za kilimwengu, mahali ambapo hali ya
kutofahamu hutamalaki, na akaweze kukwea na kuingia Mimani mwa
Mungu. Makusudi ya Mungu ni kuwanunua wanadamu wote na
kuwakusanya tena Mlimani wake Mtakatifu Sayuni, mahali ambapo
walianguka kutoka.
Kununua
huku kuna maana gani? Kunamaanisha kuwaleta watu wake kutoka
uharibifu hadi mahali pa Baraka, yanena kuhusu wokovu, kulindwa,
kuwekwa muhuri, kufunikwa naye, urejesho, kupendwa, kuonyeshwa
rehema nk. “Ndio”, hawa wamenunuliwa kutokana na wanadamu na
wakakwezwa kutokana na hali iliyodhoofika ya mwanadamu wa
kijinsia kuingia katika hali ya umilele ya wana wa Mungu. Watu
hawa wa uzao spesheli sio watu wa jinsia ya wanadamu wa
ulimwengu wa kawaida. Uzao wao hauwezi kunakiliwa kutoka kwa
ratiba ya uzao wa wanadamu, wao wanaishi kutokana na uzao wa
Melkizedeki ambaye hana baba wala mama.Wameshinda minyororo na
pingu za uharibifu na kupaa kwa uhuru na usafi war oho zao.
Wanapojitambua tena ndani ya utukufu wa Baba yao kwa kununuliwa
kwao kwa damu ya Mwana-Kondoo, hawa waliofanyika haki wa Mungu
wanaenenda wakifanyika dhihirisho la utukufu wa Mungu duniani
kote ili wote wakawatizame. Wanafanyika ishara na vibango vya
kuashiria ili kila mwanadamu waone, waamini na kubadilika kuwa
kama mfano wa Mwana; wanafanyika kuwa wakombozi wa wana wengine
walio kwenye vifungo vya uharibifu na kifo. Hali yao ya kukwezwa
na kutukuka katika Kristo inawafanya wao kufanyika makuhani wa
milele wa Mungu aishie, na wanafanyika mpito na daraja kati ya
wanadamu na Mungu Baba yao; na wanatamalaki na kutawala kama
wafalme wakieneza uzima na haki kwa wanadamu wote.
Warumi 8
19 Kwa maana viumbe
vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa
Mungu. 20 Kwa maana viumbe vyoe pia vilitiishwa chini ya
ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye
aliyevitiisha katika tumaini; 21 kwa kuwa vuimbe vyenyewe navyo
vitawekwa huru na kutolewa kaika utumwa wa uharibifu, hta
viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.
Kama ushawahi kujionea
sinema maarufu ya Uamerikani iitwayo "Superman", ushawahi basi
chungulia katika mipango ya umilele ya Mungu; wale wanadamu
waliozitengeneza sinema kama zile hupatiwa maono fulani ya
kiungu hata bila yao kujua na kuyaleta yale maono mazito na
kweli za kiroho kwa njia iliyofichika kwa wanadamu. Sinema
yenyewe huanzaje? “Ni tai, ni ndege, la, ni Superman”. Mungu
anauinua Mwili wenye viungo vingi unaoonyesha na kufanya kazi
zile haswa zinazofanywa na yule ‘Superman’ kwa ile sinema. Kazi
za kutetea kweli, haki na uhuru wa wanadamu wote, kutenda kazi
nzuri za ukombozi na kudhihirisha nguvu za Mungu kwa utukufu
wake Baba.
Johana 1
12 Bali wote waliompokea
aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio
jina lake; 13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya
mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
Wengi wamesoma sura hii na mstari huu kwa biblia, lakini
hawajauelewa kwa hakika. Nguvu ya kufanyika mwana wa Mungu ni
mamlaka na uhuru wa kutenda kwa uhakika kama Mungu hapa duniani.
Ni maana kuwa, kuwatizama hawa wasimamao Mlimani Sayuni, ni kama
kumtizama Yeye Pekee Mungu; hamna mwanadamu ambaye ashawahimwona
Mungu
Baba kimwili, lakini hawa wana wa Mungu wanamdhihirisha –
wanamfunua akaonekane.
JINA LA BABA KWA VIPAJI VYA NYUSO ZAO
Katika maono yake,
Yohana pia aligundua kwamba Jina la Baba lilikuwa limeandikwa
kwenye vipaji vya nyuso za watakatifu ambao walikuwa
wamenunuliwa kutokana na uso wa ulimwengu. Ndugu zangu, kuna
majina mawili tu yaliyotajwa kuwa yameandikwa vipajini mwa nyuso
za watu; nayo ni – Mhuri - Jina la Baba, na mhuri wa Yule mnyama
– jina la yule nyoka wa zamani ambaye ni yule mnyama. Hatupaswi
kutishwa na ukubwa wa maneno kama ‘yule myama’, ‘nyoka yule’ ama
‘joka lile’ ambayo yametumika mara kadhaa ndani ya kitabu cha
Ufunuo, kwa sababu, yote hayo yaashiria mambo mengine tofauti.
Kwa majina haya, ni mwanadamu ambaye anaashiriwa akisimama kama
uzao wa Mungu ama uzao wa Shetani.
Mhuri wa Yule mnyama ni
ujumbe ambao unaweza tu tajwa katika kijitabu hiki. Wakati ule
tu mwanadamu alilila lile tunda la maarifa na ujuzi wa mema na
mabaya, ambalo lililetwa kwake na yule nyoka (mwerevu kuliko
wamyama wote wa mwitu), aliandikika ile nambari ya yule mnyama.
Ile nambari ya yule mnyama ni sambamba na ile hali ya yule
nyoka; twayaona haya katika Mwanzo kwa sababu yule nyoka ndiye
aliyekuwa mwerevu kuliko wamyama wote wa mwitu ambaye
aliwaandika wanadamu kuanzia Mwanzo katika kuasi kwa mwanadamu.
Kuanzia pale hata hadi siku hii tulioko, kiburi, na hisia ya
kujiona imekuwa hli ya ukawaida wa mwanadamu, aliiridhi dhamiri
ya dhambi inayoasi, inayoashiriwa katika Mwanzo na uchi wa Adamu
mbele ya uwepo wa Mungu. Na ndio maana Yesu, bila kuchanganya
maneno akawaita wale waliompinga uzao wa nyoka, kumaanisha kuwa
walikuwa na mhuri wa yule mnyama juu yao.
Kuanzia wakati ule wa
uasi wa mwanadamu, yeye amekuwa akikwepa na kuuondokea uwepo wa
Mungu na akaupoteza uweza, mamlaka na uridhi kama mwana wa Mungu
katika nuru. Tulichoshuhudia katika shamba la Edeni ni
mwanadamu, akishuka kutoka kilele cha uwepo wa Mungu Mlimani
Sayuni kuingia katika uvumbi wa dunia mahali ambapo yule nyoka
alitawala. Katika uhai, mwanadamu huvalia umbo na mfano wa mtu
wa mavumbi. Jua kwa hakika kuwa lile fumbo la majaribio ya Adamu
na kuasi kwake, anapojiambatanisha na cha kimwili na cha jinsia,
yeye hukana kwa yale matendo uungu wake, ambao na huru,
usioharibika na wa milele, kuanzia Mwanzo.
Lakini twashukuru Mungu kwa sababu, kupitia damu ya Mwana
Kondoo, tuna njia ya kurejea kwa utukufu ambao wote wameupotea
kupitia Adamu, huo utukufu usiodhoofika wa Baba uliopotewa
kutoka misingi ya dunia. Kila mtu leo amepewa neema ya kutosha
ya kumsababisha kupaa kutoka vilindini mwa dunia, hata kwa Mlima
Sayuni mahali ambapo utukufu wa Mungu na uwepo wake uko na
waishi. Huo muhuri wa Yule mnyama ulioko kwenye kipaji cha uso
ambao wakati wote umemhusisha mwanadamu na Shetani na ufalme
wake usio haki hufutwa na jina na hali ya uzima wa Baba
unafuniliwa, ukiwa umechongwa kwenye kipaji kile kile cha yule
mwanadamu.
Muhuri wa Jina la Baba
ulioko kwenye kipaji cha uso inamaanisha kutembea katika ile
hali ya kiungu, ambayo ni njia inayokubalika mbele zake Mungu; ;
kwa jina hili pekee ndilo mwanadamu anaweza kwalo kujitwalia
yaliyo yake Baba.Yeyote anayetafuta kuingia kwenye yale malango
ya Ufalme wa Baba kwa jina lolote linguine atasimamishwa pale
malangoni kwa usemi, “Sikujui, wewe mtenda maovu”. Kwa jinsi hii
Roho asema, “je kuna mbwa”, na, “hakuna kitiacho najisi ama
kisemacho uongo chaweza ingia uzimani”.
Ujue ya kwamba ramani
halali na ya ukweli ni kwamba mwanadamu ni umbo na mfano wake
Mungu; “na huu ndio mwanzo wa maumbile a Mungu”. Inamaanisha
kuwa wanadamu wote kwa ukweli wana hali ya Baba imechongwa ndani
ya uutu wao. Hii yaweaonekana nguvu kutafakari na hisia za
kiwanadamu kwa sababu ya uchafu uliommeza mwanadamu, lakini
yafungue macho yako na utaona hiyo hazina iliofichika ndani
chombo hiki kinyonge na hafifu cha udongo.
Kiroho,
unawezaifananisha kipaji cha uso na nia ya ndani ya mwanadamu;
Roho anasema iweke kando nia ya kimwili na ukkaweze kubadilika
na kufanana haswa na ile nia ya Kristo, ambayo ndio ya Mungu.
Ukitaka kuuona uzima, kila mwanadamu lazima aweke nia ya
kiwanadamu ambayo, kama lile joka la dunia ni chukizo dhidi ya
Mungu, haliwezi kujua mambo ya ukweli wa umilele wa Mungu. Kuwa
na nia ya kiwanadamu inaashiria kifo kwa sababu inamkinga
mwanadamu kutokana na uhakika wa Ufalme wa Kiroho wa Mungu,
usioonekana, kumfanya yeye kugaagaa kwenye giza, kunako wingi
kilio na kusga meno. Upande wa pili, kipaji cha uso
kilichochongwa Jina la Baba ni nia ya kiroho ya Kristo, ambayo,
bila, hakuna mwanadamu ataona ukweli wa uzima wa milele na
amani. Kwa Jina hili tu, mwanadamu anawezakuvumbua tena njia
nyembamba na nyoofu iingiayo Shambani Edeni.
Warumi 8
6 Kwa kuwa nia ya mwili
ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. 7 Kwa kuwa ile nia
ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitiisheria ya Mungu,
wala haiwezi kuitii. 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza
Mungu. 9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi
hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote
aspokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
Sasa twawezaona kwa
uhakika kuwa mwanadamu katika uasi wake anajiambatanisha nay a
kidunia na huishia katika mtego wa hali ipitayo ya muda nay a
wakati. Katika ile hali a uasi, mwanadamu hufanyika mfungwa wa
uharibifu, anapouondokea ule uzima wake na hali yake ya kibingu,
katika mfano wake Mungu aliye Muumbaji, na kuambatana na hali ya
kilichoumbwa. Lakini neema imetujilia leo, kwamba kila mwanadamu
anawezatizama mifano inayoonekana kupitia Yesu msalabani na ajue
ya kwamba ni hali yake ya uanadamu, iliyodhoofika inayotiwa kifo
msalabani, ili utukufu wa Mungu aishiye ikadhihirike. Kwa imani,
wacha kila mwanadamu aisikiaye sauti ya Baba akainuke na
kurejelea lile Jina Moja la Baba, kwa kuwa mtiifu kwa mwito wa
kufa kwa mtu wa kale.
KUTEMBEA KATIKA JINA LA BABA
Nguvu ya kuweka hai na
kupa uhai iko ndani ya Baba, na Baba amempa Mwana uwezo, kwa
sababu Mwana hutembea katika Jina la Baba na hufanya lile tu
alionalo Baba akifanya.
Yohana 5
20 Kwa kuwa Baba ampenda
Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; hata na kazi
kubwa zaidi kuliko hizo atamwonyesha, ili ninyi mpate
kustaajabu. 21 Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha,
vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao.
Yohana 5
25 Amin, amin,
nawaambia, Saa inkuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya
Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. 26 Maana kama
vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na
Mwana kuwa na uzima nafisini mwake. 27 Naye akampa amri ya
kufanya hukumu kwa sababu ni Mwna wa Adamu.
Wanaoenenda katika jina la Baba ni wale waliomjua Mungu wa
ukweli na aisjie, na kuishi kwa ajili Yake kuwapa Mkate na radhi
waliopotea katika ulimwengu huu. (1 Yohana 2:13-14). Wao hufanyika
wanaopeana uzima; wakiwa wameondolewa na kuangamizwa hali yao ya
kijoka, inayotafuta maovu na mauti, ka hivyo kudhihirisha hali
ya Baba Yao ambaye ni upendo na Uzima wa milele. Hawa, kati ya
mia na arobaini na nne elfu wanaenenda kama Baba, wakiwaita wana
waliotapakaa duniani humu kama yatima, kwa sababu wao
wanafanyika Baba kwa wasio baba na Mama kwa wasio na mama.
Kristo aliyefufuka hii hali ya Baba iliyokuwa ndani mwake,
alipowaita wanafunzi kula naye.
Yohana 21
5 Basi Yesu akawaambia, Wanangu, mna kitoweo? Wakamjibu,
La….9 Basi waliposhuka pwani, wakona huko moto wa makaa, na juu
yake pametiwa samaki, na mkate…12 Yesu akawaambia, Njoni mfumgue
kinywa. Wala hakuna mtu katika wale wanafunzi aliyedhubutu
kumwuliza, U nani wewe? Wakijua ya kuwa ni Bwana. 13 Yesu
akaenda akautwaa mkate, akawapa, na samaki vivyo hivyo.
Yesu
hakwenda sokoni kuutwaa mkate, wala hakwenda kutega samaki.
Samaki waliokuwa makaani na mkate walitwaaliwa kutoka zile
hazina za kimbingu ilizo ndani ya Baba; na ni Neno la Uzima.Ni
Baba anawapa Mkate wa Ufalme wamawe ambao walikuwa wametawanywa
kaika ziwa la wanadamu. Siku Mpya inapokucha, Baba anatokea na
kuleta joto, kufariji na kutosheka katika mioyo ya wanadamu
waliokata tama usiku kucha ndani ya shimo lililojaa mchafuko
(ambalo ni ulimwengu huu ulio.)
Wanaohitimu mahali pale katika mlima ule mtakatifu, wanasimama
kama Baba ulimwenguni, kama vile Yesu alivyosimama kama Baba
wakati wa huduma yake. Basi mtu awezauliza, na si Yesu alisema
usimwite yeyote baba ulimwenguni? (Mathayo 23:9). Ukweli
ni kwamba, hawa walioko Mlimani Sayuni hawako duniani tena,
mbali wako mawinguni na huishi kule; na sio wanadamu hafifu
tena, kwa sababu walipotwaaliwa kutoka ulimwenguni (duniani),
walifanyika viumbe vipya, vilivyofanyika kulingana na umbo la
kimbingu ambalo ni Mungu Baba.
Kudhihirisha Baba ni huduma iliyokabidhiwa watakatifu naye Yesu,
aliposema, Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi,
kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa
kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. (Yohana
14:12).
Hapo mbeleni, Tomaso alikuwa amemwuuliza Yesu amdhihirishe Baba
kwa wafuasi, na Yesu akawaambia peupe kwamba ni Baba waliyekuwa
wakimwona; ilikuwa Mungu Baba alikuwa akijidhihirisha kupitia
Mwana. Haya yote yanaenda kuonyeshakwama Yesu alitembea katika
Jina la Baba, sio jina la mwanadamu hafifu. Hii ndiyo ile hali
ya ukweli ya kila mwanadamu ambaye anahuishwa kuingia kweli, kwa
sababu katika uhuisho huu, mwanadamu kwa hakika tena hufanyika
dhihirisho la Mungu asiyeonekana hapa duniani. "Alieniona
mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?”
(Yohana 14:9).
Hii haimanishi nikaenende jiani na mtaani na kupaza sauti, “Mimi
ni Baba”, na pia haimaanishi nijitaalie neno Baba mbele ya jina
langu. Huu nu ukweli tunaojihifadhia ndani mwetu na kumwacha
Roho kuufunua huu ukweli kwa wanaotutazama. Wengine wetu
wanawezashuhudia kuwa tumeingia mahali na makusanyiko ambapo
hatukujulikana, lakini tupafichuliwa na watu waliotabiri,
wakisema: “Baba wa mayatima”. Hii ni ishara ya
mwito wa juu sana na umewekwa huru na bure kwa kila mwanadamu
aliyetawanyika ulimwenguni huu.
MABIKIRA NA MATOASHI ROHONI
Katika maono,
waliotwaaliwa kutoka ulimwenguni wanaonekana Mlimani Sayuni kama
bikira.Mafunzo na dini Fulani hufananisha hawa na watu Fulani
spesheli ambao haajawahi fahamiana kingono na mwingine; dini
zingine hutumia haya maandiko kuunda mafunzo yawakatazao watu –
waume kwa wake kutooa. Twamshukuru Mungu kwa nuru ya ukweli wake
ambayo hutokana na Roho wake katika siku hii. Kama umekumbana na
hizi roho zinazopinda maandiko ili kutengeneza mafunzo yao
potovu, wewe oma kile anasema kuhusu hawa bikira.
Cha kwanza kutizama ni
hiki, hawa walikuwa ni waume, ambao hawakujipaka najisi
na wake, kwa hivyo ni bikira. Katika hali ya ukawaida, huwa ni
tofauti, sivyo? Kumaanisha, ni wake ambao hujulikana kama
mabikira kwa kutojinajisi na wanaume. Inamaanisha kuwa hawa
walikuwa wanaume ambao walifanyika matoasi kwa ajili ya Ufalme.
(Kina dada wasomao hili, hawapaswi kuona kana kwamba nazungumzia
wanaume kama vile wanavyojulikana ulimwenguni, kwa sababu hakuna
kike wala kiume katika Kristo. Hicho kikundi cha mia na arobaini
na nne elfu kina wana, kike na kiume ulimwenguni huu tulio).
Yesu alinena kwa ufupi
kuhusu hawa wanaofanyika matoashi kwa ajili ya Ufalme:
Mathayo 19
11 Lakini yeye
akawaambia, “Si wote wawezao kulipokea neon hili, ila wale
waliojaliwa. 12 Maana wako matoashi waliozaliwa hali hiyo toka
matumboni mwa mama zao; tena wako matoashi waliofanywa na watu
kuwa matoashi; tena wako matosahi waliofanya kuwa matoashi kwa
ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neon hili, na
alipokee."
Yesu kwa uhakika asema
kwamba sio wote wanawezakubali haya isipokuwa waliojaliwa na
kuchaguliwa. Yesu asema hivi kwa sababu alinena kwa lugha ya
kiroho ambayo waliokombolewa wangeielewa.
Kunena kiroho, mabikira
na matoashi (wanaume tasa) ni wale walioamua kujiweka kiroho na
kutotiwa nira na mipango na mapambo ya kilimwengu wakati huu
tulio. Hawa wamejiandaa kuolewa na Bwana na ufalme wake
uliositirika pekee. Nasema uliositirika, kwa sababu hali ya nia
ya kimwili haiwezi kuuona huu ufalme wala kuuelewa. Mungu ni
Roho na ufalme wake sio ule unaokuja kwa kutizama na hali za
kimwili – ni kamili ufalme wa kiroho. Wanaousaka huu ufalme,
lazima watembee kikamilifu wakiuzingatia ufalme wenyewe.
Waliogizani hutembea kulingana na ulimwengu huu tulio, wa
kijinsia na kimwili na wao husaka utukufu wa wanadamu na na
ulimwengu huu ulio chini, lakini wale walio na na ufunuo hakika
wa ufalme waMungu hutembea wakiwa na uhusiano na Baba ambay
uwepo wake uko sirini, ukiwa umefichika kutokana na watu wa
enzi hii tunayoishi.
Huku ndiko kupanda
katika roho ambako tumekusikia miaka hii yote, Mungu ni Roho;
kutembea katika Mungu ni kupanda katika Roho. Hii ndio maan
waona katika mistari fulani katika Ufunuo wa Yohana, sura ya
kumi na nne, ikisema kuwa wao wanamfuata Mwana Kondoo popote
aendapo.Macho saba ya huyu Mwana Kondoo humwona Baba pekee na
ufalme wake na sio kingine chochote. Hawa mabikira wa kiroho
wameunganika kwa Bwana kikamilifu na kwa hivyo hawana kauli yao
wenyewe wala nia yao wenyewe, isipokuwa kufanya mapenzi ya aliye
kichwa chao (Kristo), ambayo ni kumpendeza Mungu na kumpa
utukufu yeye amabye kutoka kwake kila mema hutiririka.
Nabii Isaya pia
akatabiri kuwahusu hawa mabikira wa kiroho (matoashi)
wanaotafuta utukufu wa Mungu:
Isaya 56
1 Bwana asema hivi,
“Shikeni hukumu, mkatende haki, kwa maana wokovu wangu u karibu
kuja, na haki yangu kufunuliwa. 2 Heri afanyaye haya,
namwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje,
auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote." 3 Wala mgeni,
aambatanaye na Bwana, asiseme hivi, “Hakika yake Bwana
atanitenga na watu wake”; Wala
toashi aseme; "Mimi ni mti mkavu." 4 Kwa maana Bwana awaambia
hivi maoashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo
yanipendezayo, na kulishika sana agano langu; 5 Nitawapa hawa
nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina,
lililo jema kuliko kuna na wana na mabinti; nitawapa jina
lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. 6 Na wageni,
walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la
Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na
kulishika sana agano langu; 7 Nitawaleta hao nao hata mlima
wangu mtakatifu, na kuwafirahisha katika nyumba yangu ya sala;
makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu;
kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote."
Unabii na kutabiri kwake
Isaya ni neno la majira tulio sasa kwa wale mioyo yao inatia
jitihada kuusaka ukombozi na wokovu wake Mungu; inaashiria watu
wanaosaka kuwa kati ya wale 144000 walio Mlimani Sayuni. Hawa
ndio watu, wanaouacha ulimwengu kuusaka utukufu wa Mungu;
wanajiunganisha na Mungu kwa imani na wanatembea katikauhusiano
kamilifu kwa Mungu wakitafuta kufanya kimpendezacho. Isaya
58 yaendelea kueleza Sabato ni nini: inanena kuhusu kuunyima
mwili anasa zake na kutenda kimpendezacho Mungu. Tunatimiza
Sabato kwa kutembea hakika kwa Roho wa Kristo. Bila Roho wa
Kristo kutuvuvia ndani mwetu, hatuwezihitimisha Sabato kamilifu
ya Mungu; ni siku kuu ya Bwana, sio ya mwanadamu.
Siku zilizopita,
watumishi walioaminika na waaminifu, ambao walikuwa na uwezo wa
kuingia vyumba vya ndani vya wafalme na watu wakuu walikuwa
matoashi. Kuwa toashi ilikuwa ni dhihirisho kwa mtumishi kuwa
amejitolea kikamilifu kutumika na kumheshimu bwana wake kwa
uaminifu. Haw matoashi walijikana vya kuwapa raha ili wampendeze
mfalme pekee, na kwa sababu ya kauli hii ya kujitolea, walikuwa
kwa kawaida wamekwezwa na kupewa kibali cha hata kuupenya uwepo
wake mfalme, na hata kula kutoka chakula chenyewe cha mfalme.
Kwa ajili ya ufalme wa
Mbinguni, kwa ajili ya Yerusalemu, kwa ajili ya Sayuni,
tumefanyika matoashi. Kama matoashi na mabikira, tumeziua hisia
zetu za kimwili, nia zetu, vitupendezavyo, kusaka tu kimleteacho
Bwana wetu (ambaye ni Roho) raha, kumpa heshima pekee; na
tunapofanya hivi, Bwana aahidi kutuleta kwa Mlima wake Mtakatifu
ambapo anatuahidi raha hata milele yote. Atuahidi sisi jina la
umilele na kilele cha furaha Mlimani wake Mtakatifu Sayuni. Hilo
jina ni jina jipya – Jina la Baba.
Siku huja ambapo
mwanadamu huanza kwa uhakika kupendezwa na mambo yanayoambatana
naye Bwana, asilegezwe tena na raha za mambo ya kimwili. Wale
wanajitalaki kutokana na raha za kimwili na kugundika na
kushikamana na maisha ya Roho, watasafirishwa mpaka sehemu ya
furaha isiyoisha kwenye vilele vya Sayuni.
WAMFUATA MWANA KONDOO KOKOTE AENDAKO
Kama kondoo waufuatavyo
unjia aupitao mchungaji, hawa walio Mlimani Sayuni humfuata
Mwana Kondoo kokote aendako, kumaanisha kuwa wanaongozwa na Roho
wa Mungu. Mtu awezajiuliza, "huyu Mwana Kondoo awaongoza
awaelekeza wapi?” Mwana Kondoo awaelekeza kurudi katika uwepo
mtukufu wa Baba mahali ambapo wanaweza tena ishi uzima wa kweli
ulioko ndani yake Baba. Wakati Yesu mara kwa mara alipokiri,
“Naenda kwa Baba”, ulikuwa ni upako ulioko ndani mwake – uitwao
Kristo, ulikuwa ukieleza makusudi Yake. Sauti iliyokuwa ikisema,
“Nifuateni Mimi”, ilikuwa ni sauti ya upako ulioko ndani
uliokuwa ukimwita mwanadamu muasi kuurejelea Utukufu wa Baba.
“Nilipo, watumishi wangu
wawepo”, kama mchungji, Mwanakondoo aziongoz nafsi za wanadamu
kwenye chemichemi za mji ya uzima mahali ambapo hawaoni kiu tena
wala kukosa lolote. Katika hali y kawaida ulimwenguni tulioko,
wanadamu katika umbo la wachungaji wa kondoo huwaongoza
wanakondoo kuelekea kwa majani mabichi, lakini katika maono ya
huyu mtume, twayaona haya ni kama yamepinda. Twaona Mwnakondoo
akiwangoza wanadamu kuelekea kwa Uwepo wa Mungu. Hili ni
dhibitisho vile hekima ya Mungu huwa ni kama upuuzi tu kwa
wanadamu wa majira tunayoishi wanaoyaona mambo kwa roho tu ya
kiasili.
Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa
Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa
kuwa yanatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
(1 Wakorintho 2:14)
Kwake Mwanakondoo wa
Mungu (Roho wa Kristo aliye ndani) ni hekima yote ya kiroho na
maarifa yake Mungu. Yohana alipomwona (Mwanakondoo) mbele ya
Kiti cha Enzi chake Mungu, alikuwa nayo macho saba yakiashiria
Roho Saba zake Mungu zilizotumwa ulimwenguni.
Ufunuo wa Yohana 5:6. Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na
wale wenye uhai wane, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo
amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na
macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika
dunia yote.
Hizi Roho saba za Mungu
zaashiria hekima iliyotwaaliwa kutoka vilindi vyake Mungu, na
kutumwa duniani kote kuwanusuru na kukomboa wanadamu kutoka
ulimwenguni. Dunia yenyewe ni kiashiria cha kiroho kuonyesha
ulingo wa mavumbi mahali ambapo kifo na kuzimu hutamalaki. Hizi
Roho saba huwanusuru hawa kwa kuwachapa muhuri vipaji vya nyuso
(nia) za wanadamu na kuwatia nuru kuwaingiza katika nia ya juu
zaidi ya Aliye Kweli ambayo hujaa kila kitu Naye Yeye Mwenyewe.
Hizi Roho saba
zawakilisha fani nyingi za hekima yake Mungu zilizotolewa
kilindini chake Mungu, na kutumwa duniani ili kuwanusuru
wanadamu kutoka ulimwenguni. Dunia yenyewe kwa hakika ni ishara
ya kiroho ya hali ya uvumbi ambapo gehena au jehanum na kifo
hutamalaki. Hivi vitu na hali hufanya hivi kwa kuchapa muhuri
kipaji (nia) ya wanadamu na kuwaangazia kuingia katika dhamiri
ya juu zaidi ya Yule aliye Kweli, Asiyeonekana, na ajaaye vitu
vyote kwa vyote.
Mwana Kondoo,
anayewakilishwa na Kristo Aliye ndani, huishi ndani ya kila
mwanadamu ambaye tu atakkubaliana na ukweli wa hali hii, na Yeye
Ndiye yale Mafuta na Sauti iongozayo, inayoelekeza wana wa
Ufalme kurejea katika hali ya kukubali kuwa wanashiriki katika
Utukufu wake Mungu. Inamfunza mwanadamu kweli zote na hubaki
ikiwa karama iliyo kuu zaidi yake Mungu kwao wanadamu, kwa
sababu bila Roho, hakuna mwanadamu anawezatambua hali yake ya
kweli katika Utukufu wake Mungu. Kila mmoja wa hawa asimamaye
Mlimani Mtakatifu wa Mungu, Sayuni, hufunzwa naye Mungu kupitia
Yale Mafuta yaliyoko ndani mwao.
1
Johana 2
27 Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu,
wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake
yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si
uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.
Isaya 54
13 Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya
watoto wako itakuwa nyingi.
Wanaosaka na kutafuta
mahali hapa pa uzima inawalazimu kuyatoa macho yao ya ufahamu na
kuyatia yale Yake Roho. Lazima waukate uguu wao uwaongozao
kusiko na waweze kutembea kwa mwongozo Wake Roho.
Mathayo 18
8 Basi mkono wako au mguu wakoikikukosesha, ukate ukautupe mbali
nawe; ni afadhali kuingia katika uzima hali umepungukiwa na
mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na
kutupwa katika moto wa milele.
9 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ukalitupe mbali nawe; ni
afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho
mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto.
Yale macho sba ya Mwna
Kondoo hufanyika macho yao ya ufahamu yawaongozayo mahali ambapo
hakuna mwanadamu wa kiasili apaelewa wala kuwezeshwa kupaelewa.
Hawa wabarikiwa huoneka na huhukumiwa na wana wa kizazi hiiki
kuwa wajinga, lkini wao kwa hakika ni wenye hekima kwa sababu
wanasimama katika mahali palipoinuka, kuutazama utukufu
uliokamilika wake Mungu.
Isaya 35
8 Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya
utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa
ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea
katika njia hiyo.
9 Hapo hapatakuwa na samba, wala mnyama mkali hatapanda juu
yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika
njia hiyo.
10 Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni
wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao
watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitkimbia.
Njia ya utakatifu katika hali hii ni njia tofauti, mpya nay a
uima ya kuishi ambayo Baba ameiwakifisha wanadamu wote
wakaipitie. Katika njia hii ya utakatifu, Aliyeko pale ni Bwana
na Bwana Pekee. Wanaotembelea njia hii waishi pekee kwa Roho.
Hli nyingine yoyote hufanyika najisi, kikwazo, na idanganyayo;
kilicho najisi na kichafu, kifanananishwacho na samba araruwaye
na kula. Hawa wanyama wote ni viashirio vya hali isiyotakasika
ya mwanadamu wa aili anayeishi kulingana na au kuambatana na
hali ya Adamu, ya damu na nyama. Hakuna njia yeyote ambayo damu
na nyama huweza kuona wala kutambua ufalme uliobarikiwa,
uliositirika wa Mungu, kuna ulazima wake yeye kuzaliwa kiroho
kupitia kufanyika upya nia yake. Ndio aweze kuishi, inambidi
mwanadamu kuingoa hali hii yake ya kuishi ya kinyama na
kujitwalia Roho wa Mungu; inambidi aone pekee kwa macho ya Mwana
Kondoo aliye ndani yake ambaye humwona tu Baba.
Mwanadamu amfuatapo Mwana Kondoo, hii humpeleka katika hatua ya
kuzaliwa upya ama kufanyika upya (katika nia) ndio ile mbegu
takatifu isiyo mawaa iliyo katika mfano wa Bwana wake itokee.
Hapa ndipo mahali pa waliokombolewa; wao huja mahali ambapo kila
hali ndani mwao hujipanga na kujisawazisha kikamilifu sambamba
na Roho wa Mungu. Kwa Roho, ile hali najisi ya kinyama
iliyokuwemo ndani ya uzao huu spesheli, pamoja na uchungu na
hofu ya matukio ya kiwanadamu hutokomea mbali, ni kana kama huyu
mwanadamu amegutuliwa kutoka kwa ndoto chafu na ishtuayo;
wanaupokea uridhi wa milele, furaha iishio ya Mungu wao.
HAWAGAIRI, KUSEMA UONGO NA HUSIMAMA BILA HUKUMU MBELE YA KITI
CHA ENZI
Kabla tuanze kutambua
maana ya Uongo, wacha tukaweze kuelewa watu wawili wanaoonekana
kuanzia siku za Adamu na Yule aliyetoka mbinguni ayulikanaye
kama Adamu wa pili - Kristo. Wacha tutambue ukweli kuwa
mwanadamu pale mwanzo aliumbika kwa Mfano wake Mungu; huu mfano
ni wa kiroho na usiounganika kimwili. Kuungamanika kwa mwanadamu
kiushirika na yule nyoka ndicho chanzo cha mwanadamu wa
kimwilitunayemuona siku hii tulio duniani. Nyoka mwenyewe ni
mfano wa fikra na nia za kimwili ambazo kila wakati
zimeshikamana na kugundika na ulimwengu; ni fikra ambazo
haziambatani na mambo ya kiroho ya Mungu. Huo umbo asili katika
mfano wa Mungu walinganika na “Chanzo cha maumbile ya Mungu”,
ama kwa maneno mengine, “Ukweli”. Uongo huja kupinga na kushusha
kweli iliyoko, na tunawezasema kuupinda ukweli. Wakati mwanadamu
anapopotea kutoka kwenye ramani ya kiungu na kuegemea kilicho
cha jinsia na cha kidunia, uongo hujitokeza, na pamoja na ule
uongo huja shida na dhiki zinazotokana na uhai uliotengeka na
Yule ambaye ni Mungu wa kweli.
Kristo ndiye Mfano wa
Mungu aishie, Yeye aliye kutoka Mwanzo; na hili ni dhihirisho la
Uzima na Uhai ulio wa kweli na hali ya kila mwanadamu hata
ingawa kwa muda mwanadamu yule anawezakuwa amepungukiwa na ile
kweli kuu. Huu ukweli umefichika ndani ya kila mwanadamu katika
hali ya uhai wake. Paulo analenga hili na anaiita hazina
isiyohesabika, ya dhamana, iliyofichika katika vyombo vya
udongo. Ufunuo huu wa nuru unang'aa leo kupitia Roho kuufunua
huu ukweli ili mwanadamu anaweza tena kurejeshwa katika ule
ushirika usiotengeka na Baba. Lango kuu la kurejelea katika
kuungamanika huku na Mungu ni mwanadamu kuamka kutoka usingizi
wake na kuutambua ukweli kuwa Kristo yu ndani mwake. Na ndio
maana Shahidi aliye ndani asema, “Mimi ndimi njia, na ukweli,
na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya Mimi”. Roho
amwelimisha mwanadamu kuhusu chanzo chake katika Mwili wake
Kristo na sehemu yake yule mwanadamu katika Ule Mwili; na huu
ndio Uzima wa Milele.
1 Yohana 5
20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye
ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani
yake yeye aliye kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo.
Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.
Uhai unaofuata mwili ndio uongo na ndicho chanzo cha uovu na
upotovu wote ulioko leo, na ndio maana Yesu asema, “Usiusumbukie
uhai wako kwa sababu wote ni bure”. Hakuna njia yoyote mwanadamu
aishie kulingana na mwili na damu awezasimama bila chachu wala
mawaa katika uwepo na utukufu wa Mungu, kwa sababu, katika hali
yake, yeye ni muasi na ni kiwiliwili tu cha umbo wa fikra zake.
Mwanadamu yeyote atembeaye kulingana na mwili na anaungama
maisha yaambatanayo na mwili ni muongo; yeye anaishi katika
udanganyifu. Kwa jinsi hii, nikinena kiroho, wanadamu wote huwa
na hufanyika waongo.
Zaburi 116
11 Mimi nalisema kwa haraka yangu, Wanadamu wote ni
waongo.
Kama, kwa upande wa
pili, mwanadamu anawezasikia manukato ya kuongea kwake Roho na
kuambatana na yale yasemwayo, kumfuata Mwana Kondoo popote
aendako, yeye ataujua ukweli na huu ukweli humfungua na kumuweka
huru kutokana na nira na pingu za kifo. Kweli ni kwamba,
utambilisho wa mwanadamu halisi ambao ni Kristo, bila chachu,
utambulisho uliofichika ndani ya Mungu; utambulisho mwanadamu
aliupoteza na kupokea gharika ya uongo na giza ya ulimwengu
tuliomo.
Wasimamao wakiwa
wamekombolewa Mlimani Sayuni hawana uongo mdomoni mwao kwa
sababu wao huungama na kunena kweli tu kutokana na Nia Yake
Roho, sio kulingana na nia ya mwili.
Ufunguo wa kweli
unaowaondolea wanadamu lawama mbele ya Kiti cha Enzi ni imani
ndani ya damu ya Mwana Kondoo na kutambua mbegu halisi na ya
kweli na ile hali ya kweli ndani mwake. Wakati umekuja na
umewadia wa kutambua mbegu hii takatifu ndani ya kila mwanadamu
na kuacha kutambua wanadamu kulingana na mwili na damu, kwa
sababu, tuendeleapo kutambuana kulingana na mwili na damu,
wanadamu hupoteza kuona kwake kwa ule ukweli na kutumbukia
kwenye mtego wa kifo. Ndio maana Mtume asema:
2 Wakorintho 5
16 Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa
jinsi ya mwili. Ingawa sis tumemtambua Kristo kwa jinsi ya
mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.
Ufunguo wa kuzitwaa
nguvu, mamlaka na imani mbele zake Mungu ni nguvu za dhamiri
isiyonajisika na kuondolewa lawama kabisa mbele zake Baba. Hili
huja kwanza kupitia mwanadamu kupambanua kweli, na uwezo wake
kuzipungia kwaheri sauti zote zipingazo kweli na imani na
kutembea katika kweli. kwa kujua kweli kumhusu yeye, kama
Kristo, atakiri, “Mimi na Baba ni Mmoja, na ni Kiungu
kisichotengana”.
Kinachodanganya dhidi ya kweli hubaki nje ya lile Jiji la
Dhahabu mahali ambapo wasiomjua Mungu huangamia kwa sababu ya
upumbavu ulio ndani ya mioyo yao unaowatenganisha na Uhai na
Uzima ulioko ndani ya Mungu. Wakati umewadia na ndio huu tulio,
ambapo mwanadamu akaujue ukweli na kuukariri ndani mwake na kwa
kila mwanadamu mwingine; kwa sababu hili hufungua Malango ya
Milele kuingia kwao Ufalme wake Mungu.
Waefeso 4
25 Basi uvueni uongo, mkasemekweli kila mtu kwa jirani yake;
kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.
WIMBO MPYA MBELE YA KITI CHA ENZI
Hebu keti na kutafakari
kwaya ya kimbingu na nzumari na zeze na sanaa za nyuzi, wakiimba
nyimbo zilizo na ukuu na uzuri wa kimbingu, ambazo hazijawahisikika
ulimwengu tuliomo. Hiki kikundi cha waliokombolewa wanaimba wimbo
mpya amabo hakuna mwanadamu angewezafunzwa, isipokuwa wale
waliokombolewa kutoka ulimwenguni. Najua kwamba kila mwanadamu
atafuta kuwa katika ile hisabu ya waliokombolewa. Ukweli ni kuwa,
mtu yeyote awezasimama katika ile hesabu, muda tu anapochukua ujumbe
huu wa Neema na kukimbia nao katika uwepo wake Mungu.
Huu ni wimbo wa
ushindikuwa wale kwenye hii hali ya Utukufu wawezauimba; hawa ndio
ndio wanaowezaimba, “Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi,
Ewe mauti, uchungu wako?”, "Bwana ni mchungaji wangu,
sitapungukiwa kitu", “Bwana ameikomboa nafsi yangu kutoka shimoni na
nitaona Nuru Yake”, “Amenifanya kuwa na furaha kuu”.
Wasimamao Mlimani
Sayuni, Eneo la kiroho lake Mungu lililoinuka, wana macho yao
yamefunguliwa kuuona utukufu na urembo wa Yeye Aliye Wa Kweli na
wanapata kujua na kushiriki vilindi vya upendo wa Mungu. Sawia na
pamoja, vinubi, zeze na nzumari ndani mwao zafunuliwa pamoja na
maumbile mengine yote kutangaza rehema zake Mungu zisizotajika toka
kizazi hadi kizazi.
Mtu awezatamani kuuliza,
“Kama wimbo ulio kwenye vinywa vya waliokombolewa ni wimbo mpya,
wimbo uliokuweko, ule mzee, ni upi”? Wimbo mzee unazungumzia
kuomboleza na kilio, kusaga meno na dhiki kuu katika ulimwengu wa
wafu ambapo mwanadamu aliuweka utanda wake na kulala pale, kwa
kutofahamu. Haya yote yanawezafupishwa na kuwa mstari mmoja, na ndio
huu, “kutengwa na ule Uhai na Uzima ambao Ndio, na uliohifadhika
ndani yake Baba Mungu”.
Msomaji wangu, inuka na
udhihirishe ile nuru ambayo wewe ndiye, leo ndio siku yako ya
ukombozi na kufufuka katika na kuingia utukufu wako. Sikiza, sikiza,
elewa na uchanganye maneno haya yaliyotakasika na imani na utatambua
tena mtu wa Mungu ambaye uliye. Unapojitembua tena vileleni vya
Sayuni, utapepea juu ya vyote na kutawala vyote. Zeze iliyoko ndani
mwako ambayo iliwekwa chini kingoni mwa mito ya Babeli ikawezeinuka
tena katika mfano wake Mungu, ikatamalaki katika ukamilifu,
Utakatifu, na bila lawama, kwa sifa za Utukufu Wake.
Zaburi 137
1 Kando ya mito ya
Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.
2 Katika miti iliyo
katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu.
3 Maana huko
waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka
furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.
Kusifu kwa kweli
hakupatikani kati ya wanadamu wa ulimwengu huu, hata kuwe na
kusifiwa na hisia gani, ni bure, na ni maigizo tu ya kidini ya
wanadamu watembeao katika vivuli vya giza. Ndio, kuna uwezekano kuwa
wewe wawezainuliwa na zile hali, lakini kila mwanadamu na afahamu
kwamba hii sio hatimisho ya kile ambacho Mungu ameweka ndani ya
mwanadamu. Sis sio wasimamao na kuwakashifu wanadamu, ila sisi
huwasihi watu wote kupaa na kukwea na Bwana katika kufufuliwa kwao,
kuhisi kuabudu kwa kweli kwa kimbingu. Ni kwa kweli, kwa kusisimua
na kusikoelezeka kwa usemi wa mwanadamu. NI KWA AJABU!!! Sababu yake
ni kuwa kila chembe ya uhai ndani ya mwili wa mwanadamu
inaambatanika na maumbile mengine ulimwenguni huu kumtukuza Yeye
Aliye Juu ya vyote.
Sifa yapatikana katika Jiji Takatifu Lake Mungu, ambalo ni
Yerusalemu ya Kimbingu, Jiji lililowekwa kwenye vilele vya Sayuni.
Hatusemi kuhusu zana za nyuzi za kijinsia bali zana za nyimbo za
kiroho zilizoko ndani ya mwanadamu. Wasimamao kati ya wale 144000
wanamwimbia Bwana kwa hali ambayo wale tu walioko kwenye nuru
wanaweza elewa pekee. Kwa hakika, ni kama nuru na rangi zake saba,
wimbo katika hali ya kawaida una sauti saba; na hizi ni ishara na
mifano iashiriayo nuru na kuelewa kunakotokana na Roho Saba zake
Mungu. Hawa ndio wanaowezauimba ule wimbo, ambao wamefufuka kwa na
kuishi kwa Roho wa Kristo ndani yao na ndimi zao zimefunguka kupitia
Roho kuona na kukiri maono ya kimbingu.
Zaburi 57
8 Amka, utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri.
Rafiki zangu, upendo gani na heshima gani inayoweza kuwepo kuliko
ukuu huu wa wokovu wa Mungu unaoletwa kwetu kwa sahani ya dhahabu –
kwa heshima kuu vile. Wokovu ambao humrusha mwanadamu hadi kilele
cha maumbile na kumfanya yeye kutembea kama Mungu machoni pa
Ulimwengu!
Bwana na akulinde.
Trevor Eghagha