KUNYAKULIWA NA KUINGIA KATIKA UPENDO
PDF
1 Wathesalonike 4:16-18.
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka
kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya
Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha sisi tulio hali tuliosalia,
tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili kumlaki Bwana hewani; na hivyo
tutakuwa na Bwana milele.
18 Basi farijianeni
kwa maneno haya.
Na hivyo tutakuwa
na Bwana milele...katika ulimwengu uliosongeka kwa shida na matatizo, isikize
sauti yake Mfariji aliye ndani na ukafarijike kuhusu tumaini hili
lililobarikiwa. Tumaini hili nalo ni la kuungamanika naye Bwana, muumba wa
mbingu na dunia. Bwana ndiye Roho anayejikusanyia mataifa yote ya ulimwengu
ambayo yamekitwa katika giza na upumbavu. Yeyote asikiaye na kusadiki ule mwito
wa kuungamanika naye Bwana ni Roho mmoja naye Bwana, kumaanisha kuwa sio wawili
tena, kwa sababu ule ukuta uliodhaniwa na fikra zao kuwa uliwatenga haupo tena
na Mungu anafanyika yote ndani ya yote. Basi tutaungamanika na Bwana
milele...kumaanisha kuwa kifo hakimo tena, kwa sababu kama aishivyo uhai
milele, hata sisi twaishi vile vile.
Furahini!!! Nami
nasema furahini, mnapoisiskia habari hii njema inayotiririka kutoka Sayuni.
Iweke hofu na huzuni mbali. Yabadilishe mavazi yako meusi ya huzuni na
kuomboleza ukayavae mavazi tukufu ya sifa. Macho yako yakilenga milima idumuyo
milele, ukafurahi kwa ajili ya Neema hii isiyoelezeka iwanyanyuwao wanadamu
kutoka masagio makali ya kifo na kuwakusanya katika ushirika wa kweli wa upendo
katika wingu lile la utukufu. Yote ni kuhusu Ushirika wa Upendo na furaha ya
milele katika mahali pa mbingu, ambamo wote waishi kwa ajili yake Bwana pekee
wakitazama uzuri wa Maumbile Yake. Huu ukweli unalinganishwa na Yerusalemu mpya
inayoshuka kutoka mbinguni, maumbile Yake Mungu yanayoingia mahali ambamo
yanawezaonekana. Mkashukuru na kufurahia. Tena nasema furahini.
Kama umeamka kwa
kiwango fulani, utajua ya kuwa usiku waisha na bambazuko laja, nuru ya asubuhi
yaingia. Nuru kuu ya ufunuo yang'aa kumfunua Mungu wa ukweli Aliye Baba wa
Upendo Aliye kati ya kila mwanadamu. Wale wanafunzi walioitambua na kuifuata
ile Nuru waliieneza ile habari njema na kutangaza kuwa "Mungu Ni
Upendo". Ndani mwao, Nuru hii iliyo safi ilikuwa imeangamiza kila uongo
uliokuweko uliosema kuwa Mungu ni wa ghadhabu na wa kujilipishia kisasi, na
asiyetulizwa na lolote isispokuwa jicho kwa jicho na jino kwa jino.
Katika upumbavu
wake na kujikaza kwake kidini, Paulo aliondoka na kuanza maangamizi yake,
kwaangamiza wale waliojaribu kuenenda dhidi ya sheria za juu juu zilizoitwa za
Musa walipomkiri Kristo. Na angefanya lipi lingine kama aliowaiga ni Musa na
Eliya na Daudi, ambao wenyewe walieneza maangamizi kupitia kile walichokiona
kuwa mtazamo wao kumhusu Mungu. Hawa watu walikuwa na nia nzuri, na walifanya
walichojua kulingana na nuru chache waliokuwa nayo. Lakini Yesu ambaye ndiye
Nuru Dhahiri yake Mungu baadaye alikiri kuwa "Nuru iliyoko ndani mwako
ikiwa ni giza, basi una giza kuu kivipi!" Wakati Nuru ya Kweli ilipomkabili
Paulo akielekea Dameski,yeye alikiri ya kuwa Mungu ni
Upendo. Alikiri kuwa Mungu Ni Mmoja na ni yote ndani ya yote. Aliiona Nuru ya
Ulimwengu.
Mungu Ni Upendo na
Ule Upendo wajaza kila kitu. Hakuna kinachopinga hili ndani ya mioyo ya
wanadamu kinawezastahimili Nuru ya Ufunuo huu unaofunuliwa na kung'aa sasa. Huu
ufunuo unaong'aa kutoka vilindi vyake Baba, ndio lile Ziwa La Moto maarufu
linalozikabili kifo na mauti, ambamo ndimo makao mwa uongo wote na mahali
ambapo mwanadamu ameweka malazi yake katika maasi yake. Nuru yake nyeupe na
miale isiyoonekana kwa macho ya wanadamu, yaangamiza kila fikra na wazo katika
njia Yake lipingalo Upendo, Upendo ambao ndio kina na moyo wa kila kitu
kilichoko. Upendo wabaki kuwa chanzo na mwisho wa kila kitu. Upendo ndio Ile
Nguvu iliyositirika na isiyoonekana kwa macho ya wanadamu, izilishazo na
kuzihifadhi sayari na limwengu lizoko.
Hata ingawa
haijulikani, na mara nyingi hupuuzwa na wengi kimakusudi, ambao wamesongwa na
mizigo ya maisha wanayoishi sasa, fani tofauti za huu Upendo zaonekana dhahiri,
zikionekana kupitia mambo yaliyoumbwa. Tukilitafakari jambo hili kuu na la
kushangaza, mwanadamu lazima ajifunze kutoka mifano ya Nuhu, Henoko, Musa na
Eliya na wengine wengi waliofunguliwa kutoka vifungo vinavyowafunga wengi ulimwenguni
tunaoishi na kuingia kwenye utulivu ambamo sauti yake mwanadamu huisha na
kubakia ikisikika Sauti yake Mungu pekee. Mwanadamu lazima aelewe kuwa alitoka
mahali hapa patulivu akiwa pweke na uchi, na itambidi ayaachiliye yote ili
kurejea kule ambako vazi lake pekee ni Upendo.
Tukinena kwa mfano,
Nuhu aliyaacha yote ulimwenguni na kukwea vilele vya Sayuni na kuvumbua mbingu
mpya na nchi mpya ambamo Upendo, uambatanifu na haki ya Ukweli zapatikana.
Henoko aliishi maisha yake kwanza kwanza kama mwanadamu wa mwili na nyama.
Lakini aliyaacha yale na kutembea naye Mungu kumaanisha kutembea naye Roho
pweke. Mwali wa moto wa Upendo ungemmeza yeye hatimaye, asijepatikana. Musa
akakwea na kuuwacha utukufu wa Misri, ambayo ni ishara ya mwili na damu na
kuupata Uwepo wa Milele uliofichika nyuma ya vinavyoonekana. Alivumilia makali
ya jangwa na miiba yake, majoka, ngee na mbweha wakali, ambazo zinaashiria
kutoamini kunakotokana na fikra na mawazo ya kiwanadamu. Kwa kuendelea kwake na
kuvumilia, alikutana na Ule Mwali wa moto wa Upendo kwenye kilele cha ule mlima
Uliotangaza Ukweli wa Mungu Aliye mmoja na Aliye ndani ya kina cha kila kitu.
Uwache Upako wa
ndani ukakuelekeze mahali pale patulivu. Lisikusumbue wala kukushawishi vingine
lolote lile. Usiondolewe kutoka safari hii ya kuutambua Upendo katika vilele
vyake Mungu. Njiani mle, msafiri anayeutafuta Ukweli itambidi asiangalie nyuma
kama alivyofanya mkewe Lutu akafanyika nguzo la chumvi ambayo ni ishara ya
mauti na utasa katika maarifa yake Mungu.
Suluhu linalosalia kwake mwanadamu, ni
kuyaondoa mawazo yake kwa mambo ya ulimwengu huu tulio, na kutojaribu tena
kuhifadhi lolote lile kwenye 'mema' yake, bali kuachilia vyote kwa ajili ya
Upendo. Ni kuwaacha ndugu, mashamba, nyumba za kifahari, na nia zote zake mwanadamu
ziambatanazo na ulimwengu tulio sasa, tukiwa na ahadi dhabiti kuwa yote haya
hurejeshwa mara mia kwa mia katika Milki ya Mbingu ya Upendo. Na uyaache ya
kale ya kilimwengu yapite na mapya ya Upendo wa kimbingu uwepo.
Katika hali hii yako mpya ya utulivu,
tafakari kwa macho yako ya ndani na utaona kuwa yote yanayodhihirika kwenye
ulimwengu huu tulio ni fumbo tu linaloimba ule wimbo wa Upendo na Utukufu wa
Ufalme wake Baba usioonekana. Wimbo huu waelezea Utukufu, Ukuu na Milki ya
Mungu aishiye. Wafunua Upendo usioelezeka, na Umoja uliopo...kutotengeka kwake
mwanadamu naye Mungu aishiye. Katika sauti tofauti za zumari na kinubi,
walioamka wasikia mstari huu wa wimbo..."...Mimi ndimi Bwana, na kando
Yangu hamna mwengine." Na "Dunia imejaa Utukufu wake..." Angalia vilindi vya nchi na sayare na
nyota, na utaona ni wingi wa Upendo unaojidhihirisha kwa njia nyingi na
tofauti.
Ukweli huu wadhihirishwa bayana katika
kichwa cha wimbo huu "Milima Ii Hai" katika sinema iliyotia
fora sana iitwayo "Sauti Ya Muziki".
MILIMA II HAI
Milima ii hai na
sauti ya mziki
Ikiwa na nyimbo
zilizoimbwa miaka maelfu
Milima yajaza moyo
wangu na sauti za mziki
Moyo wangu wataka
kuimba kila wimbo usikiao.
Wakati Richard
Rogers aliuunda ule wimbo wa ile sinema "Sauti Ya Wimbo", hakujua
alikuwa anaingia kwenye mashina na vilindi vyake Mungu. Bila ya kujua, mtunzi
huyu alinena kuhusu Ukweli ulio wa jadi katika Milki yake Mungu. Miaka elfu
(karne) katika milima inaashiria Milki yake Mungu ambayo yajulikana pia kama
Siku Ya Bwana. Milima ya milele ya Sayuni ii hai na sauti za nyimbo, na kila
mmoja aishiye kwenye ule mlima amejihami kwa kinubi cha dhahabu wakipiga wimbo
maridadi wa kumtukuza Aishiye milele. (Ufunuo 1:1-3). Ule umaridadi wa wimbo
unafananishwa na ule wa wana wa Mungu, wale nyota wa asubuhi wanaotajwa kwenye
vyuo vile vya kale vya Ayubu, walioimba kwa furaha na kwa pamoja wakati misingi
ya ulimwengu ilipowekwa (Ayubu 38:4-7).
Ikisomwa tu kwa
mawazo ya kiwanadamu, Ayubu 38 yaonekana kana kwamba ni hadithi tu ya
kihistoria, lakini sio vile hasha. Inafunua Ukweli uliopo hata kupita muda na
wakati...ushirika wa kiungu unaomiliki na kutawala katika Mungu mbinguni.
Wawezaliita Kanisa la Mzaliwa wa Kwanza ama Kusanyiko lake Mwenye Nguvu Sayuni.
Hii ndiyo nguvu ya limwengu zote. Kama huu Ushirika wa Upendo kwenye vilele
vyake Mungu haungekuweko, hakuna kitu kilichoko kingekuwa. Ni kweli mbingu
zatangaza Utukufu wake Mungu.
Zaburi 19:1-4.
1 Mbingu zahubiri
Utukufu wake Mungu, na anga laitangaza kazi ya mikono yake.
2 Mchana husemezana
na mchana, usiku hutolea usiku maarifa.
3 Hakuna lugha wala
maneno, Sauti yao haisikilikani.
4 Sauti yao yaenea
duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. Katika hizo ameliwekea
jua hema.
Katika andiko hili,
mbingu zaashiria kusanyiko la wana wa Mungu, nyota za asubuhi au malaika wote
wakitangaza makuu ya Utukufu wake Mungu. Na haya yote ni katika mambo
yanayoonekana. Kilele cha uhusiano huu wa mapenzi na kuabudu katika mbingu,
vitu vilivyoumbwa hutokea na kuonekana. Nguvu za Upendo katika kusanyiko hili
huumba na kuzihifadhi chembe zote zifanyazo sayare, nyota na ulimwengu mzima.
Ni kweli
inayotambulika kuwa Mungu alizifanya mbingu na dunia na kila kitu kupitia mtu
mmoja wa kimbingu tumwitaye kwetu sisi Kristo. Lakini kweli hii sio kamili usipotambua
kuwa wewe ulikuwa ndani mwake kabla ya misingi ya ulimwengu, na kabla ya kitu
chochote kudhihirika. (Yohana 15:27). Inamaanisha kuwa mwanadamu umwonaye
akitembea pembeni alikuwa Roho Moja na Bwana kabla ya kushushwa kwake katika
huu mwili unaojihisi kuwa umetangwa na Mungu. Ulikuwa ndani yake kabla ya ujuzi
huu tuuitao ulimwengu wa mwili na damu. Ulikuwa ndani Yake kabla ya kufanyika
chini ya malaika au wana wa Mungu katika ulimwengu tulio. Ulimwengu tulio ni
matunda tu ya upumbavu na kutoelewa kuwa mwanadamu amekitwa katika Uhai Mmoja
Wake Mungu na ndio Kristo. Wewe ni Muumbaji pamoja na Mungu katika Kristo. Wewe
ni Kazi yake kwa kweli. Hili linatuondolea hekaya tulizoziamini kuwa Kristo ako
mahali fulani kule nje amejitenga nasi. Kristo ndio ule Mwili wa Mbingu ambao
ndani Mwake ni kusanyiko lisilohesabika la jeshi la Mbinguni. Hiki ndicho
chanzo chake mwanadamu katika Utukufu.
Kuungamanika huku
kwa mwanadamu na Mungu kwaonekana katika wimbo ule wa mapenzi unaodhihirishwa
kama mti na matawi yake, ama mwili na viungo vyake. Bila matawi, mti haupo. Na
bila viungo, mwili haumo. Sayare na nyota kule juu zadhihirisha kusanyiko hili
la kilimwengu katika vilele vya Nguvu na Milki yote mbali na kupita vikwazo vya
muda na wakati.
Mambo kama haya
yawezasikika kama hekaya na hadithi tu kwa yule anayesikia, ambaye amezoea
kusongeka na vilivyo vinyonge na vidhaifu vya ulimwengu wake mwanadamu wa mwili
na nyama. Lakini kila mtu aamrishwa kutega sikio ili kusikia na kumruhusu Roho
Tulivu kumwongoza tena kwenye mahali pake katika Huu Mwili. Nuru ya Ufunuo
yang'aa tena leo ili kumwamsha mwanadamu katika Ukweli kuwa YEYE NI KIUNGO
MUHIMU KATIKA KRISTO, AMBAYE NDIYE MWILI WAKE MUNGU. Upumbavu uliopo kulihusu
hili jambo hakuwezi kulifutilia mbali. Ni Kweli na ya kudumu. Baba awakumbusha
wanawe kuhusu vilele walivyoanguka kutoka, na atafuta njia ya kuwarejesha
katika hali tukufu ya wanawe Mungu na nyota za asubuhi walizo. (Ufunuo 2:5).
Imenakiliwa
kimakusudi kuwa pale mwanzo, katika maumbile yake Mungu, nyota wa asubuhi WALIIMBA
PAMOJA na wana wake Mungu walishangilia wote kwa furaha. Roho wake Mungu afunua
Umoja na Upendo ulioko katika Roho. Kwa kweli, ni vyema kiwango kipi ndugu
wakiwa pamoja katika Umoja. Upako wa uzima humiminika kwao, amani na furaha
bila kipimo (Zaburi 133). Umoja huo mkamilifu hupatikana tu kwenye vilele vya
Sayuni, Milki iliyoinuka ambamo ndio makaazi yake Mungu na huko ndiko
kunakosalia tumaini lake mwanadamu ambaye anawezapambanua Kweli leo. Katika
mahali hapa palipoinuka, mwanadamu huishi kupitia Kweli katika hisia
zilizoinuka mahali ambapo ataona na kutembea tu katika uhusiano na Mungu na
Ufalme wake pekee. Ili kuufikia Utukufu huu uliomkwepa mwanadamu, lazima
ajizoeshe katika Kweli na akaweze tena kujuana na mambo yasiyoonekana yake
Mungu. Mambo haya ya Mungu ni ya kutoonekana tu kwa muda. Mwanadamu anapoamka
kikamilifu katika hisia zake ndani, yaliyoonekana kuwa siri zake Mungu
yatafanyika ufunuo bayana.
Yeye asema, "Nitaja
niwakusanye, ili NILIPO nanyi pia muwe" (Yohana 14:3). Huku ni kule
kuyakusanya mataifa yaliyotawanyika na kuyafanya Moja, ambalo ni Kristo. Ndiko
kule kukusanya kusanyiko la zile nyota za asubuhi na wana wa Mungu Mlimani
Sayuni, mahali palipoinuka, makaazi yake Mungu. Mataifa yote yatatiririka hadi
vilele vya Sayuni na yaungamanike tena na kuwa Mmoja na Kristo. Hili
limezungumziwa sana kuhusu kurejea kwao waliokombolewa Mlimani Sayuni. Katika
kuungamanika huku kwa kiungu, kunao ule Uzima na Nguvu ziumbazo na kuhifadhi
kila kilichoko.
Na kwa wengi
walioupata huu ufunuo wa Kristo, amewafanya kuwa wana wake Mungu na kwa hiyo
wamepata unjia wa kuingia katika lile kusanyiko la wote katika Mwana (Yohana
1:12). Roho pia asema, "yeyote ashindaye nitampa ile nyota ya
asubuhi" (Ufunuo 2:26-28). Kwa maneno mengine, ashindaye uogo wa shetani
kuwa yeye ametengwa na Uzima na Utukufu wake Mungu, nitampa nyota ya asubuhi
ili akang'ae tena katika Utukufu kama jua ling'aavyo. Matendo tofauti yake Roho
wake Mungu kati yetu leo, yasaka kutukusanya wote turejee katika Umoja wa Imani
vileleni mwake Mungu, mahali ambapo Uwepo wake na Baraka zake zisizo kipimo
huishi.
Kwa muda mchache,
Yesu angefunua hii Milki ya ushirika wa Mbingu kwa wafuasi wake watatu
alipobadilishwa mlimani fulani uliotengwa. Ili kufika pale, iliwabidi wasafiri
siku tatu wakipitia njia milimani zenye ukiwa na mawe makuu. Na zile njia
zaashiria mapito yake yeye anayerejea palipo patulivu. Walipofika pale, macho
yao kwa muda yalifunuliwa kuona Milki isiyoonekana yake Mungu na Uzuri wake.
Dhibitisho la hili laonekana kupitia yule mfuasi aliyetamani sana kubakia pale
baada ya kuonja furaha na Utukufu wa Uwepo wake Mungu. Kwa kweli hakuna awezaye
kuuonja Uwepo wake Mungu na kusalia alivyo. Kileleni mwa mlima ule, walimezwa
na kufunikwa kwa wingu lenye Nuru ya Utukufu, na kutoka kwalo sauti ikaguruma
na kukiri, "Huyu ndiye Mwanangu mpendwa, msikieni yeye".
Sadiki kuwa,
waliona onyesho dhahiri la kusanyiko nzima la watakatifu au wana wa Mungu
katika Nuru. Lile wingu lenye Nuru ya Utukufu sio lingine bali ni lile Wingu la
Mashahidi walioungamanika na kuwa Mmoja na Baba. Mwana wa Mungu alikuja kufunua
hii Milki kwao wanadamu na kuwakusanya wao kurejea katika Ushirika huu. Hii
ndio siri ya Ushirika uliofichika katika Mungu kabla ya misingi ya ulimwengu
lakini sasa yawekwa dhahiri kupitia Injili (Waefeso 3:8-9). Ni Ushirika
mtakatifu wa Upendo na Umoja wake Baba na Mwana (1 Yohana 1:13). Na ni vyema
kwako kutambua kuwa hiki ndicho chanzo chako wewe. Awaye yeyote yule
anapotambua chanzo chake ndani yake Mungu, pale pale atajua Mwisho. Kwa sababu
Ufunuo huu ndio Nuru ya kukufungua wewe kutoka kwenye vifungo vyake yule muovu.
1 Yohana 5:19-20.
19 Twajua kuwa sisi
tu wa Mungu, na dunia yote hukaa katika yule mwovu.
20 Nasi twajua ya
kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue aliye wa
Kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa Kweli, yaani ndani ya Mwana wake,
Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa Kweli na Uzima wa milele.
Musa naye Eliya
walionekana katika lile wingu. Hili laonyesha kuwa Torati na Manabii wote
walikuwa mashahidi wa hili kusanyiko la Mbingu, wala sio wa mipangilio na
miundo ya kidini tuionayo ulimwenguni tulio sasa. Kama unachokisikia kila
wakati hakishuhudii kuwa sehemu yako ipo katika lile kusanyiko la wingu, basi
dini yako ni tupu na imekwisha kufa.
Kufikia utimilifu
wa kusanyiko hili la kiungu, nia zetu lazima ziweze kukwea na kupaa juu
zikayaache ya mwili na damu na kuyaingilia ya kimbingu. Hii yaashiriwa naye
Yesu aliposafiri safari ya siku tatu ili akifikie kilele cha ule mlima pamoja
na wafuasi wake. Wale ambao wangependa kuuonja uzuri wa Uwepo itawabidi wapae
katika Nia yake Kristo kutumia mabawa yake Roho.
Yesu yule yule
aliyeomba akisema, "Baba, nitukuze mimi kwa UTUKUFU WAKO, Utukufu ule
niliokuwa nao kabla ya misingi ya ulimwengu", alinyakuliwa katika lile
wingu la Utukufu alipokuwa akimalizia huduma yake duniani ili kuonyesha ramani
ya kutukuzwa wale walioitwa kushiriki katika Utukufu wake Baba. Ili maneno yake
yatimie aliposema, "Narudi kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na
Mungu wenu", Yesu aliingia katika lile wingu la Utukufu na kufanyika
Mmoja naye Baba. Lile wingu ni dhihirisho la Utukufu wake Mungu. Mwanadamu
awaye yeyote aliye na upambanuzi haswa atajua kuwa faraja yake na kuzawadiwa
kwake kuko katika hili wingu la Utukufu. Watu wote walitoka katika hili wingu
la Utukufu na WOTE LAZIMA WARUDI KULE. Hii ni kwa sababu hili wingu linaashiria
Chanzo na Hatima ya KILA KITU.
Wingu hili la
Utukufu lasimamia kusanyiko la kimbingu la watakatifu katika Bwana. Katika
kusanyiko hili, Bwana yupo. Lilipo kusanyiko hili, Bwana yu kati yao. Wao na
Bwana ni Mmoja na hawawezi kutenganishwa. Kwa mifano na mafumbo, Roho afunua
mwelekeo huu tena na tena haswa wakati Musa alipowaongoza wana wa Israeli
kutoka Misri kupitia jangwa ili kuingia nchi ya ahadi. Mungu alijifunua kati
mwao haswa kupitia wingu mchana kwa kusudi moja la kuwaelimisha na kuwakumbusha
watakatifu kuhusu kuungamana waliokuwa nao naye Mungu kabla ya misingi ya
ulimwengu. Na kama vile wana wa Israeli walivyobatizwa katika lile wingu, kwa
njia ile ile awaye yeyote yule asikiaye na kumakinika katika Kweli, hubatizwa
yeye pia katika wingu ijapokuwa ni lile wingu haswa lisiloonekana la Utuku wake
Mungu.
Yasikie maneno yake
Mtume Paulo, "Tutanyakuliwa panoja nao katika mawingu, ili tumlaki
Bwana hewani; na hivyo tutakuwa na Bwana pamoja milele. Basi farijianeni kwa
maneno hayo". Bwana Asifiwe!!
Elewa hivi...Kule
kunyakuliwa katika mawingu ni kule kunakoitwa katika maandiko mengine
KUFUFULIWA KWA WAFU. Watanyakuliwa kurudi tena kuungamanika nao Mwili wa Bwana,
kwa sababu kuungamanika kwetu hakika ni kwa kiungu katika Bwana. Yote haya
hufanyika katika nia zetu wale wanaousikia mwito wake Bwana kupitia Mwili wake
wa Wajumbe au Mitume au kwa maneno mengine, Malaika Mkuu.
Usikawahitarajia
kuyaona haya yakionyeshwa kwenye runinga na stesheni maarufu ama kupitia redio.
Hili ni jambo litendekalo vilindini mwako wewe binafsi na kuendelea hata
milele. Mambo ya kiungu huwa na yataendelea kufichwa kutokana na ujuzi wa
maarifa ya kiwanadamu, na kupitia kufichwa huku, ulimwengu umeshindwa kuelewa
kufunuliwa Kwake. Wanadamu bado hawajaelewa Ukweli wa Milki yake Mungu
isiyoonekana inayofunuliwa hata wakati huu tulio. Haigharimu tena ishara kwenye
mbingu kama ilivyokuwa zama zile. Leo hii, mwito wetu wa kusanyiko sio kwa mlima
fulani uliozungukwa ma mawingu kama ilivyokuwa siku yake Musa wakati wana wa
Israeli walipotembea katika mafumbo na vivuli, badala ya kutembea Nuruni ya
Kweli ambayo ni Sayuni, makao yake Mungu Baba milele. Kilicho cha Mungu haswa
hakionekani kwa mwili na nyama lakini chadumu milele.
Kaisome mistari hii
kwa umakini na ukaelewe alichofundisha Roho kupitia waraka wake Mtume Paulo:
Waebrania 12:18-23.
18 MAANA
HAMKUFIKILIA MLIMA UWEZAO KUGUSWA, ULIOWAKA MOTO, WALA WINGU JEUSI, NA GIZA NA
TUFANI.
19 NA MLIO WA
BARAGUMU, NA SAUTI YA MANENO; ambayo wale waliyoisikia walisihi wasiambiwe neno
lo lote lingine.
20 maana
hawakuwezastahimili neno lile lililoamriwa. Hata mnyama akiugusa huo mlima
alipigwa kwa mawe.
21 Na hayo
yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na
hofu na kutetemeka.
22 BALI NINYI
MMEUFIKILIA MLIMA SAYUNI, na MJI WA MUNGU ALIYE HAI, Yerusalemu wa mbinguni, na
majeshi ya malaika elfu nyingi,
23 mkutano mkuu wa
kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu
wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika.
Yashike haya kutoka katika hii mistari:
1. Siku tulizo, Mungu hawakusanyi watu
kwa mlima wowote uonekanao kwa macho, na ulio na miali ya moto na giza na moshi
kama tufani. Hawakusanyi watu kenye kelele za tarumbeta kama ilivyokuwa kule
Sinai. Kukusanywa kwetu hakutambuliki kwa macho ya mwili...ni hali ya kiroho.
Ni kukusanyika kunakofanyika pasipoonekana kwa macho ya mwili kwa wanaoisikia
sauti yake Roho siku hii.
2. Kukusanywa kwa mkutano huu ni kweli
iliyoko kwa wale wanaowezatambua hili kwa sasa, wala sio tukio lijalo wakati
fulani wa siku za usoni utakaoashiriwa na ishara fulani huko nje. Kama Paulo
asema kuwa yeye alifikilia lile kutano kwenye lile wingu la Utukufu Mlimani
Sayuni, inastaajabisha vile wanadamu wazitafuta ishara ambazo wanasema
zitatukia siku zijazo usoni. Mtu awaye yeyote yule anaweza kupaa wakati wowote
ule, hata sasa hivi asikiapo sauti ya tarumbeta (ujumbe wake Bwana).
Na Ujumbe huu wa tarumbeta wasema nini?
Ujumbe ni kuwa kuna mwito wa kukusanyika kwake Mungu katika lile wingu la
Utukufu Mlimani Sayuni.
Hili hufanyika mwanadamu anapoisikia
Sauti ya Roho wa Bwana iitwayo TARUMBETA katika maandiko ya biblia. Ni Sauti ya
Roho inayowakutanisha watu kwake Yeye. Kumbuka kuwa Bwana Mwenyewe ndiye Ile
Roho (2 Wakorintho 3:17).
Wakati Mtume Paulo alipoandika waraka
wake maarufu kwa ndugu Wathesalonike akizungumzia kile wengi wanachokiita
KUTOWEKA, alijaribu kuwakumbusha upya na kuwahimiza waliokuwa wamechoka tayari,
kuhusu Tumaini La Mwito wao. Kutoka ule waraka ni dhahiri kuwa Mtume Paulo
alikuwa anawazungumzia mambo ambayo walikuwa wameyajadili pale mbele wakiwa
naye. Huu ulikuwa ni waraka kwao ndugu wenye imani kama yake Mtume na
walioelewa lugha aliyokuwa anazungumza kupitia ushirika waliokuwa nao hapo
mbeleni. Hakuna Mthesalonike wa kawaida angeelewa ayasemayo Mtume Paulo kama
hangekuwa ametiwa Nuru ya hekima ya kimbingu.
Tangu siku ile Injili ilihubiriwa,
Mbingu Mpya na Nchi Mpya zimefunuliwa machoni pao wanadamu, na wanaofuatilia
wakaimiliki hii Milki Mpya katika Kristo wanena kwa ndimi mpya, usemi mpya, kwa
maneno mengine. Katika maono ya wale Mia Na Arobaini Na Nne Elfu,
waliokombolewa duniani na kusafirishwa hadi vileleni mwa Mlima Sayuni, hili ni
dhahiri. Hawa wanalo jina la Baba vipajani mwa nyuso zao na wanena kwa ndimi au
lugha ambayo hakuna yeyote duniani aielewa. Yamaanisha kuwa wao wana nia mpya
na mawazo mapya...yake Babao...na wanena lugha yake Mungu..ambayo
ndiyo pia Lugha Ya Roho.
Hili latendeka sasa hivi wanaposadiki
wale wanaoamshwa na ule Mwito, kwa kuwa wameufikilia Mlima Sayuni, Yerusalemu
ya kimbingu, Ulimwengu ambao wakusanya kila kitu kwake Mungu. Lugha wanayoongea
nayo hawa roho waliokombolewa haiwezi kamwe eleweka kwa akili za walio wa mwili
na nyama. Twaonywa kuwa tusikawahitarajia anayefikiri kupitia kwa maarifa ya
mwanadamu atapokea taarifa itokanayo na watakatifu walio katika Nuru. Kwake
yeye taarifa ya Roho ni upumbavu.
Fikiria kwa makini, Yesu aliyazungumzia
mambo ya Ufalme kwa ndimi za Roho na mambo haya aliyoyanena yalionekana na
wingi wa umati kama hekaya na mafumbo tu. Lugha yake ambayo kwa undani wake
twaielewa ilileta majibizano mengi na mvutano, na kwa kweli haikueleweka hata
kwa wale waliokuwa makuhani wakuu wa dini siku zile. Wakati Nikodemo
alipomuuliza Yesu, "mtu mzima awezaje ingia tena tumboni mwa mamake na
azaliwe tena..." kwa kustaajabishwa na lile swali, Yesu alimuuliza
"mwalimu mkuu kama wewe Israeli na kweli ndogo kama hii hauielewi.."
Hili linaendelea katika dini tofauti tofauti ulimwenguni hata wa leo. Watu
wengi hawaielewi taarifa ya Roho kuhusu tumaini la dhamani la Imani waliyoitiwa
wala hawaioni njia panda iliyowekwa mbele yao wazi kuwapeleka Uzimani.
Lakini kati ya haya
yote kulikuwa na kundi dogo lisilo na sifa zozote ambalo macho yao ya ndani
yalifunguliwa wazi kuona kikamilifu na kuielewa taarifa yake Yesu. Na hiyo ni
kweli hata sasa. Baadaye Yesu aliwaelezea waliotafuta upambanuzi zaidi kwa nini
ilimpasa Masihi aseme kwa mafumbo katikati ya umati, lakini awafafanulie zaidi
waliomsaka sirini na awaelezee mambo bayana. Yesu alijibu virahisi na kusema,
"Kwa walio nje - yaani walio gizani, yote yapeanwa kwao kwa mafumbo. Heri
kwenu kundi dogo mwayaona na kuyasikia yaliyowapita wa kale na watawala wa
kizazi hiki".
Yesu yule yule
ndiye anayezungumza kupitia Roho katikati ya watu wake walio na masikio ya
kusikia. Kwa hivyo wanadamu wanapaswa kuwa makini ili kutambua nyakati na mambo
wanayoyasikia ili wawe waridhi wa wokovu huu mkuu unaofunuliwa sasa. Wanadamu
wanafaa kuwa makini wasifuate njia walizofuata wale waliomsulubu Yesu kwa
upumbavu wao. Kama mwivi gizani usiku, mjumbe wake Mungu huja na kuwahabaria
walio na masikio ya kusikia siri ya Ufalme wa Mungu. Lakini kama tujuavyo,
wengi huukataa.
Shida ya mwanadamu
ni kuwa amekosa kusikia. Na kiroho ni kama aliyekufaganzi. Hauelewi Utukufu
wake unaoambatana na mambo yasiyoonekana ya Ufalme wake Mungu. Mpango kamili wa
ukombozi, ambao pia waitwa Urejesho Wa Kila Kitu ni kumtambulisha kila
mwanadamu kwa ule Utukufu alioupoteza uliopo ndani yake Mungu. Tangu siku zile
Neema hii iletayo wokovu ilipotangazwa na kudhihirishwa kutoka mbinguni, Baba
anena kuhusu kwa usemi ulio sawa kuhusu wokovu huu uliowekwa wazi kwa kila
mwanadamu. Baba hatazungumza tena katika mafumbo na kwa mifano vivuli kama
alivyonena zama zao Musa na za manabii. Kila mtu na akatulie na kuisikiliza
Sauti iwaongozao wanakondoo kurejea zizini mwao. Hata Musa aliyekuwa mtumishi
mwaminifu katika mambo msingi aliyoyapokea, alitangaza kupitia Roho kuwa Baba
atamwinua mwanadamu duniani, naye ndiye mtakayemsikia.
Kumbukumbu LaTorati
18:15, 18.
15 Bwana Mungu wako
atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; MSIKIZENI
YEYE...
18 Mimi
nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia
maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.
Miaka mingi
baadaye, Mungu angetia dhibitisho Lake La Kibali kwake Yesu alipoguruma toka
mbinguni alipotangaza, "Huyu ndiye Mwanangu pekee niliyependezwa naye,
MSIKIENI YEYE". Twanenewa na yale yale kupitia Roho...ambaye ndiye
Upako ulio ndani, lakini wengi kwa kutoelewa wamening'inia kushukilia sauti ya
Musa na kukosa kuisikia Yake aliyetiliwa Muhuli wa Kibali Wake Mungu.
Wakati uliopita,
tuliyasikia mambo kimafumbo tu, na kwa njia ya kuashiria, basi ikatulazimu
kutembea kama walio gizani na kujiundia matumaini yasiyoafikiana na mbinu za
kidini za kujaribu kumfurahisha Mungu aliye na hasira zisizotulizika. Lipi
ambalo wanadamu hawajawahifanya kujaribu kumtuliza Mungu na kuingia vitabu
vyake vyema (kama anavyo), kwa ajili ya vile tulivyomwona Mungu? Damu za kafara
za watu na wanyama, mahema na mahali wakfu pa kuabudia, mipangilio ya kuabudu,
vuvio huku na kule, mikutano ya mahema, mikesha, mavazi fulani, ibaada za
batizo, matoleo tofauti tofauti, tohara sio haba, kustahimilisha miili uchungu,
kutokula na mifungo tofauti tofauti, njia tofauti za kuomba na kutafakari n.k.
Mwanzo mwanzo, njia
hizi zake mwanadamu alizozivumbua yeye zilionekana kana kwamba zilimwelekeza
mahali fulani mpaka alipovumbua kuwa alikuwa anakimbilia tu mzunguko duara
akiwa amefunga macho, akidhani kuwa yumo safarini. Macho yako yalipofunguliwa
ulitambua kuwa hukuwa umesogea hata hatua moja, ilhali ulikuwa umechoka sana.
Kuhamia makanisa tofauti au kuwatafuta wachungaji watakaokulisha ilionekana
kama yatenda kazi, lakini baadaye ukajua haikutenda lolote. Ukombozi wa kweli
na kutosheka hakukuwadia..safari za kutafuta hili na
lile hazikwisha. Safari zilizoelekea kukosa tumaini zaidi...shimo la giza, kwa
maneno mengine.
Kwa kutumia maneno
yake Mtume Paulo, hawa ni wale wasomao lakini wasije kuutambua Ukweli. Haya ni
yale mawazo yazungukayo kwa mviringo usioisha wa kidini. Manabii wa kale wa
Waazeki na Wamisri walisikia lakini kwa kivuli tu na wakajenga minara mikuu ya
pembe tatu wakijaribu kuufikia Uungu, ingawa baadaye walitambua kazi zao
zilivyokuwa nyonge. Vile vile wayahudi walijenga hekalu lililokuwa la
kushangaza sana zama zile. Walitenda hili wakidhani pengine kupitia hili
wangepata kukaribiana naye Mungu. Hasira iliwajaa Alipokuja Yesu na kusema
"Mimi Ndimi Hekalu". Wafuasi wake wakaja baadaye na kukiri, "Sisi
ni Hekalu Lake Mungu".
Bila kutambulika na
wengi, hizi itikadi zimefurika na kujaza kila mfumo wa dini leo. Haya ni
mafuriko yaliyojaa uongo uliozificha funguo za maarifa kutoka kwa wengi
watafutao Ukweli. Uongo huu huisha wakati mwanadamu anapoanza kuisikiliza Sauti
Yake Roho. Kusikiliza ni kama kupokea ule Ufunguo Wa Daudi ufunguao malango ya
jela za kifo na mauti. Kwa kuisikia kweli tena, nafsi kama ndege hupata mwanya
wa kutorokea kutoka kwa mtego wake mnasaji na kuingia kwenye uhuru mtukufu wao
(M)wana wake Mungu...Huru tokana na dhambi...huru tokana na hofu na kifo.
Wanadamu wataelewa
lini matamshi yake Yesu, "Mimi Ndiye Ufufuo", "Mimi Ndimi
Uzima", "Mimi Ndiye Mwanzo", "Mimi Ndiye Mwisho",
"Mimi Ndiye"? Unaelewa huu msemo, "Uzima Umewadia"?
Ni wakati mwafaka wake mwanadamu kuwacha wazo lake Matha aliyekuwa amekolezewa
kasumba ya imani fulani kuwa kuna ufufuo wa kimwili utakaofanyika kule nje
wakati fulani ujao. Wakati Yesu alipouliza swali, "Waamini nduguyo
Lazaro atafufuka tena?" Matha alijibu, "Ndio naamini atafufuka
tena siku ile ya ufufuo". Dadake huyu Lazaro kama watu wengi wa kizazi
hiki aonyesha fikra za wengi ambao waamini kuwa kunayo siku ambayo waliokufa
watafufuliwa na kuingia utukufuni. Wakati umewadia na ndio huu tulio wa
kuisikia Sauti yake Baba ikiongea kupitia mdomoni mwake Yesu na kutangaza kuwa
hakuna tukio kama hilo lijalo siku fulani ya usoni, bali asema, "Mimi
ndimi ufunuo na Uzima wa milele".
Sauti hiyo isahihishayo yake Yesu ilikuwa ilifukuze pepo la upumbavu na
kutoamini kutoka kwa kila mwanadamu atakayenyenyekea na kusikiliza.
Leo hii ule Uzima
ni dhahiri kwa kila mtu kuona. Mwanadamu anahitajika kusikia kwanza, halafu
kuutambua Uhai huu Mmoja. Ni kuutambua huu Uhai kama Uzima wako na kwa imani
kuamka na kurejea katika Uzima huu. Mwanadamu akikosa kusikia, yeye huikataa
Neema impayo wokovu, na huendelea katika safari yake ya mviringo wa utupu. Kwa
sababu hii, tunawasihi kuwa ikiwa bado leo, ukiisiia ile Sauti dhahiri,
tusiifanye mioyo yetu kuwa migumu na kufa katika kutoamini kama walivyo wengi
wa umati kule nje. Jiambatanishe na Sauti ya Ukweli na ukaingie katika pumziko
lako la Utukufu.
Usijisumbue
kutafuta ishara na maajabu ya nje, wala kugaagaa jangwani ukidhani kuna msaada
kule. Usitazame Mashariki ya Kati ukitumaini kuna kitu kitatendeka kule, ama
unabii fulani, zote hizi zitakutoa kutoka kilicho kweli. Usidanganywe na vitabu
vilivyoandikwa na mababe wa fani za masomo wa siku hizi, kwa sababu kile tu
watakachokifanya ni kukuondoa kwenye kweli iliyo na uwezo wa kuiokoa nafsi
yako. Unachohitaji ili kukusafirisha nafsi yako iliyo kama ndege kurejea
Shambani mwa Bwana ni kuisikiliza Kweli. Kile Baba anachoweza na atakachofanya
ni kutangaza Ukweli uliofichika kutoka kwa ufahamu wake mwanadamu tangu misingi
ya ulimwengu. Hili laleta uamsho kwa wana wa Mungu ambao wamekufa na kuzikika
katika hali ongo ya mwili na damu wakitengeka katika mawazo yao kutoka kwa
Uzima tele upatikanao ndani Mwake Roho.
Kama Lazaro, kila
mtu atahitajika kukubali jiwe lililo moyoni mwake lisukumwe na liondolewe ili
akaweze kusikia Sauti yake Baba ikisema, 'Mwanangu, Toka kaburini'".
Hilo jiwe lawezakuwa ni imani unazozituza ulizojiwekea kama hazima ya kiungu
ama iwe ni itikadi na tamaduni za jadi za wanadamu ambazo hukufanya ujihisi u
mmoja na wengine katika mipango yao bila kujiona katika mpango wake Mungu.
Yaache haya yaende na utamsikia Baba akizungumza, na sio tena kwa mafumbo. Kama
wangoja kama Matha kuwe na tukio fulani siku ya usoni, wewe umefungiwa kaburini
ukitembea katika nuru fulani ambayo kwa hakika ni giza.
Wakati vikwazo
vimfanyavyo mwanadamu kutosikia vinaondolewa, anasikia mlio mkuu unaoleta
ukumbusho wa mambo aliyoyasahau. Mambo kuhusu mahali pake pamoja na nyota za
asubuhi na kuutambua Ukweli kuwa Yeye Ndiye. Kweli Kuu hung'aa tena, naye
hufunguliwa kutoka vifungo vilivyomtia pingu maishani ya mwili na damu.
Kuitambua na kuielewa ile Kweli ndiko kunakoleta uponyaji na ukamilifu wa
watakatifu. Hadi sasa, ishara za nje zinazoambatana na mitazamo ya vitu
vilivyoko nje hazijanawirisha maisha ya wanadamu hata chembe, na hata
hazijawavuta wao hata hatua moja kuusogea Ufalme wa Mungu. Kama hizi ishara
zingekuwa ndizo, wana wa Israeli waliyoyaona makuu kupitia mkono wake Musa
wangeingia uzimani, lakini haikuwa vile. Hata makusanyiko waliyomfuata Yesu
hawangenufaika na kupokea cha Kweli kwa sababu hawakulenga kushika habari
ambazo Yesu alipeperusha.
Cha maana kilikuwa
ni kuisikia Kweli, na kwa sababu hiyo, maneno haya, "Tilia maanani
unavyosikia kile Roho anachosema na kanisa" yaenda tena na tena kwa
wote wakao ulimwenguni huu. Sauti ya Roho ndio ile Tarumbeta iitanayo
ikiwatafuta wana wake Mungu waliolala ili kuwaamsha na kuwarejesha na
kuwahifadhi kwenye Utukufu wake Baba. Hii Sauti yasambazwa kupitia mwili wa
wajumbe na watenda kazi (au Malaika Mkuu) ambao wameungana kwa kusudi moja na
Bwana kueneza Sauti hii ya Roho kwa wanadamu wote.
Wanapoisikia Sauti
hii, au mlio huu, au tarumbeta hii, siri yake Mungu inakamilika, na ule msemo
usemao, "...na wote watanijua kutoka aliye mdogo hadi aliye
mkuu..." unatimilika. Na huu ndio Mwisho. Wanadamu wote pale hatima
watapambanukiwa kuwa walichokiwaza kumhusu Mungu kilikuwa tu ni fundo la moshi
wa mawazo yao yatokanayo na moyo uliotiwa giza. Katika Uamsho, mwanadamu huanza
tena kutembea na kuishikilia nafsi yake ikiwa ndani yake Mungu.
Yesu aliliweka hili
dhahiri aliposema, "Kumjua Mungu na Mwanawe uliyemtuma ni Uzima wa
milele" (Yohana 17:3). Maarifa haya
yamepita maneno tu na kuyapita mawazo duni kumhusu Yesu aliyezaliwa na mwanamke
fulani. Inakubidi uwezeshwe kuona kwa undani ili kuelewa hili. Kama kifurushi
kilivyo, maarifa ya Mungu na Mwanawe huambatana moja kwa moja. Ukimpata Mmoja
hata yule mwingine itakubidi uwe Naye. Kujua wanavyojumlishwa ndio Uzima wa
milele. Kumjua Baba ni lazima umjue Mwana, na Mwana sio mwingine ila ni Kristo
aliye ndani mwako. Kwa kweli hakuna awezaye kumjua Mungu bila kujijua yeye
mwenyewe...Mwana Katika Kweli. Kupitia ufunuo huu toka juu, anayedanganya,
ambaye ni Shetani, anafungwa na minyororo na huangushwa kama radi na kuingia
kwenye shimo la giza kumaanisha kuwa hatakuadhiri tena milele.
Huu Ukweli wa
kiungu uliofichwa katika chombo hiki cha udongo ndio njia pekee kuelekea kwake
Mungu, kwa kuwa Yeye Ni Mmoja na Baba. Katika hali yake halali ya kukwezwa na
uamsho, yeye ndiye Baba, Mungu Aliyefichika ndani ya mwili wa damu na nyama wa
mwanadamu wa ulimwengu huu. Jina 'Ulimwengu' lamaanisha upumbavu wa kutoielewa
siri yake Mungu na yake Mwanadamu. Lakini Ulimwengu huu huisha wakati mwanadamu
huamka na kutambua kuwa yeye ni kiungo katika Mwili wake Mungu. Mwanadamu ni
dhihirisho duniani Lake Mungu asiyeonekana. Haya ndiyo maarifa yanayotangazwa
na ile Tarumbeta inayomwinua mwanadamu hadi hatima ya Kweli kuwa yeye ni mmoja
na Mungu asiyegawanyika na asiye na uharibifu.
Ukweli huu
huzivunja nira za tamaa na humwamsha mwanadamu katika tabia asili ya Mungu
aishiye ndani mwake. Yeye hutambua kuwa hakuzaliwa kupitia mwili na damu, na
kuwa uhai wake ni wa kutoka milele, kabla ya kudhihirika hapa uliwenguni huu
tuuonao kwa macho. Yeye hukumbuka kuwa ni Mmoja na Muumba wake na sio mmoja na
kilichoumbwa, na kwa lile yeye hutiwa nguvu ya kuvishinda vyote akutanavyo
navyo katika ulimwengu huu wa mambo yapitayo.
Katika Uamsho huu,
mwanadamu hukusanywa na kurejeshwa katika kusanyiko la kimbingu la roho
zilizokamilika katika Mungu na huimba katika kutaniko la Mwenye Nguvu pamoja na
Sauti za maji mengi wakisema, "Dhambi, wapi uchungu wako? Mauti, wapi
ushindi wako?" Sauti ya maji mengi inayorudirudiwa katika kitabu cha
Ufunuo ni kusanyiko lile la watakatifu katika lile wingu la Utukufu. Lile wingu
ni unyevu unyevu wa maji yaliyotiwa Uhai yaliyokusanyika na kupaa kwake Mungu
na huishi kwa ajili yake Mungu na huongea kwa Sauti yake Mungu. Wao huongea
pamoja kama ngurumo kuu, na ndio maana waitwa Wana Wa Ngurumo.
Sauti ile ya maji
mengi ndiyo ile ile iliyotembea (yaani kushiriki) katika shamba la Edeni.
Katika uasi, huu ushirika ndio Adamu alioupoteza. Katika hali yake ya chini ya
uasi, Adamu hangeweza tena sikia na akasahau mahali aliposhuka kutoka, kati ya
miili ya kiungu na Utukufu wa lile wingu. Akazisahau nyimbo za Sayuni
zilizotangaza, "Mimi ndiye niishiye, na kando Yangu hamna
mwengine". Akasahau kuutafakari Uhai wa Muumba wake. Na basi akapoteza
nguvu za kushinda mauti.
Yohana 14:26.
26 Lakini huyo
Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu,
atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Bwana asifiwe.
Tarumbeta au Sauti ya Roho ii hapa kutukumbusha tuliyoyasahau katika kaburi la
usingizi wake Adamu. Roho wake Mungu kama umande uiloweshayo ardhi na pumzi
yake Mungu kupitia Tarumbeta zile, zatia Uhai ndani mwake mwanadamu kupitia
kukumbuka kumrejesha katika utukufu wa Milki ya Edeni. Kwa kukumbuka, mwanadamu
akwea tena na kurudi kwenye wingu la Utukufu na kujijua tena kati ya miili ya
kimbingu ambazo ni zile nyota za asubuhi.
Leo Mwito umetoka
wa kumtoa Adamu kutoka mavumbini ya mauti na kaburi na kumuungamanisha tena
katika ushirika mtamu wa kusanyiko la ulimwengu mzima katika lile wingu. Bwana
Mmoja, Mwili Mmoja, Roho Mmoja, Mungu Mmoja na Baba Mmoja Amefunuliwa na
kukusanywa kwetu ni Kwake Huyu Mmoja.
Amka...Amka na
ukajitikise toka kwenye mavumbi, ukajivike mawazo ya Roho na ukaungamanike na
Bwana. Yaanza kwanza kwa kusikia halafu kujinyenyekeza kwenye Kweli hii kwa
kukiri. Mawazo yetu lazima yaambatanishwe tena na yake Bwana ili kutembea na
kunena kama yeye kwa sababu Yeye ndiye ule Uhai. Jitambue wewe kama Yeye Aliye
Juu, na kwa imani ukachukue nafasi yako katikati ya mashahidi wengi katika lile
wingu. Ukajifunze kuongea na Sauti ya maji mengi kati ya yale mawingu
yanayokiri Jina La Bwana.
Ile pazia
imeharibiwa milele na mlango uliofunguka kuwekwa wazi mbele ya kila mwanadamu
ili aingie ndani na kushiriki katika Ushirika wa Upendo na furaha katika wingu
la Utukufu. Roho asema na kila mwanadamu PANDAA HATA HAPA JUU.
Baraka.
Trevor Eghagha.