[.:ENGLISH:.|.:ITALIAN:.|.:FRENCH:.|.:SWAHILLI:.|.:HINDI:.    
 
 


 

News letter subscription
   
Name
Email
 

 

 

 

 

 

 

 

 

KUHAMISHWA KWAKE HENOKO

PDF

 

Kupitia andiko hili, tunataka kutazama siri ya kuhamishwa kwake Henoko, ili asije akona mauti; na pia tutaona jinsi ushuhuda wake una manufaa ketu sisi katika wakati huu tunaoishi. Mafunzo kama haya ambayo yanagusia uungu na hali ya kutokufa huwakanganya wasomi wengi kule nje nan i kwa sababu maswala haya hayazungumziwi hata kidogo katika fani tofauti tofauti za kidini na hata za filosofia na imani za kibinadamu. Wanadamu hawaisikilizi sauti tulivu ya Roho wake Bwana, kwa hivyo wanasongwa na mambo yanayotokana na kelele za kule nje, badala ya kuisikiliza ile sauti inayowezanusuru nafsi zao.  Wao hubebwa na mawimbi ya maarifa na imani za kibinadamu. Dini haina uhai inaoweza kumpa mtu yeyote; maarifa na usomi wa kisayansi hayana uzima. Anayewezampa mwanadamu uzima  ni Roho wake Bwana, na ndio maana tunahimizwa kusikiliza  kwa makini, kwa sababu kupitia kusikia tunahamishwa kutoka giza lililoko nje ambalo laitwa Dunia katika maandiko, kuingia katika Nuru, ili tuwezeishi kwenye Nuru kama Yeye Bwana (Mwana Wa Mungu) alivyo katika Nuru. Tunaposikiliza kwa uvumilivu, ile hali yake Mungu inatufungukia sisi, na tunapita kutoka Kifo hadi Uzima, kutoka ufukara wa kiroho unaomwandama mwanadamu wa mavumbi na kuyaingilia makuu ya utajiri usioeleweka bayana wake Mwana Wa Mungu toka Mbinguni.

 

Cha kushangaza kuhusu mambo yote yanayohusiana na uungu, utajiri wa Uzima wa kweli, na kunawiri kwetu, ni kwamba yanapatikana bure kwa wote kupitia Roho wake Bwana. Lakini kwao wanadamu waliofichwa katika nia zao na utukufu batili wa kilimwengu, hawawezikuona mbali. Hawawezi kuingia katika maono yao katika mambo yale yasioonekana kimwili, na kwa hivyo mambo yale hayawezikuwa ya maana wala manufaa kwao. Wanadamu huyapenda sana matunda Yake Roho Wa Bwana (ambayo ndio Mti Wa Uzima), lakini hawapendi kuambatanishwa na ule Mti wenyewe usioonekana; wao hupenda kuambatanishwa na ule mti mwingine unaoonekana kwa macho (mti wa maarifa ya mema na mabaya) ambao unaashiria mtu wa kijinsia na maarifa ya kilimwengu, lakini wakati ule ule wao huchukia matunda ya kifo yanawoletwa na ule mti. Roho wake Bwana yupo, na anabisha kwenye milango ya mioyo ya wnadamu ili aingie na ale pamoja nao ili awape kile kitakachhowavusha kufikia vilele vya Utukufu waliposhuka kutoka, ndio waweze tena tamalaki juu ya nguvu za kifo zilizoko tu kwenye fikra zao (Ufunuo 3:20-21).

 

Tukiyazungumzia kuhusu manufaa ya kusikiliza, tafadhali soma mistari ifuatayo itokayo kitabu cha Isaya:

Isaya 55:1-3.

1 Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila dhamani.

2 Kwanini kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu ni kitu kisichosibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.

3 Tegeni masikio yenu, na kunijia; SIKIENI, NA NAFSI ZENU ZITAISHI; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.

 

Uwezo wetu wa kutega sikio ili tusikie ndio itatufanya sisi kuridhi rehema za Daudi zilizotajwa kwenye mstari wa tatu. Na hii ni ashirio la kinabii la Baraka zinazoambatanishwa na Kristo na Ufalme wake. Twaliona hili pia katika Zaburi 89:20-37. Ahadi zake Mungu za milele kwa Mwanawe anayetamalaki milele kwenye Kiti Cha Enzi ni hizi…Kutokufa  na Ushindi Hakika Dhidi ya Maadui wake wote. Twajua kuwa Adui wake Kristo muhtasari wake ni huu…KIFO NA MAUTI, kwa sababu imeandikwa, adui wa mwisho kushindwa ni kifo chenyewe (1 Wakorintho 15:26). Hizi Baraka zinaenea hadi kwa Mwili wake ambao ni Kanisa, kwani asema, Kifo na Mauti haviwezi kulishinda Kanisa lake (Mathayo 16:18) Wakati Yesu anamwelezea Petero kuwa malango ya kuzimu hayatalishinda Kanisa lake, anamaanisha ‘ekklesia’ kumaanisha WALIOITWA KUTOKA. Hawa ni wale waliokusanyika kutoka gizani na upumbavu ambao unaitwa kwa ujumla DUNIA, na kufanyika mwili mmoja ujulikanaao na Mungu Mwenyewe, na unaoitwa KRISTO. Inatubidi kuipata picha haswa kulihusu Kanisa hili lake Mungu; ni Mwili wake Kristo ama tunawezauita ule Mwili Mkusanyiko wa Kimbingu  wa Waliokombolewa wake Bwana. Sio majengo wala mafunzo ya kidini. Kuna uwezekano tutakusanyika katika majengo fulani KWA MUDA TU, lakini usipoteze hili akilini kuwa ni KUKUSANYIKA NA ROHO ZINGINE KATIKA KANISA LA ALIYE WA KWANZA LILILOKO MLIMANI SAYUNI, MAKAZI YAKE MUNGU YASIYOONEKANA. Hapa ndipo mahali pa Baraka na Uzima usio kipimo; Milki ambayo Kristo alikuja kutukusanya tuweko.

 

Tunapopata kuingia mahali hapa palipoinuka, kile tunachohitajika kufanya tu ni kuyafungua masikio na kusikia Ukweli kama Roho Anavyotufunulia; ni kama kuupokea Mkate Wa Uzima kutoka kwake Bwana Mwenyewe. Awaye yeyote aagizaye Mkate (Neno La Roho) kutoka kwake Baba, kwa moyo wake wote, ataupokea bure kwa kuwa Baba hamnyimi yeyote kilicho Chake; Mapenzi Yake Mema ni kupeana Ufalme wake na Lote Alilo na Alilo nalo kwa wanadamu wote. Tulipokuwa watoto tulinena na kutenda kama watoto, lakini lisaa laja, na ndilo hili tulilo ambamo lazima tuondokee mambo yote ya kitoto na kutazama mambo yaambatanayo na uzima wa Milele. Inatubidi kuyaondokea mambo yote ya kijinga ya uwanadamu na kuanza kusikiliza kwa makini maneno ya hekima yanavyotiririka kutoka kwenye vilindi vyake Mungu Baba.

 

Tafakari letu na ombi ni: BABA, YAONDOE MACHO YANGU TOKA UBATILI NA UNIHUISHE KWENYE KWELI YA NJIA ZAKO. UFANYE MOYO WANGU KUAMABTANISHWA SAMBAMBA NA NJIA ZAKO NA SIO KWA NJIA ZA KIJINGA ZAKE MWANADAMU. YAFANYE MACHO YANGU YAWE KILA WAKATI YAMELENGA UWEPO WAKO, KWA KUWA WEWE NDIYE KILA KITU KILICHOKO. NIFUNZE HEKIMA YAKO ILI NIWEZETEMBEA KATIKA NJIA ZAKO NA NIKAWEZEYAFUNGUA MACHO YANGU NIKAONE SIRI KUU KATIKA NENO LAKO. AMINA.

 

Tukakumbushwe kuwa Mwana wa Mungu ameshuka toka mbinguni kama NURU YA ULIMWENGU na Ametupa roho wake ili atuangazie na Nuru ya Uzima hadi wakati hakutakuwa na chembe yoyote ya giza. Kristo ametufunulie Nuru ya Kweli na Uzima, aliporarua vuli kuu na pazia lililokalia mataifa ya ulimwengu huu tuliomo, na pale kuukaribisha Ulimwengu Mpya ambamo nafsi zetu zi hai katika Mungu Aishiye. Katika hii Njia Mpya na iliyo Hai, hali ya kuishi kama wanadamu waliotengwa na Mungu imeisha, kwa sababu tumepata urejesho kwake Mungu ili tuwe mmojaNaye Aishiye Milele. Ndani mwake ni Nuru na hamna giza hata kwamwe. Madhumuni ya Injili ni kutukusanyisha Kwake Yeye, hamna linguine. Ukilisikia linngine, jua kwa uhakika kuwa hiyo sio Injili yake Bwana wetu Yesu Kristo. Hapa ndipo mahali (ama milki) ambapo Kristo ameandaa, ili sisi ambao tumetega sikio ili kusikia, atukusanye kwenye Mahali hapa penye utele wa Uhai na Uzima na hakuna chembe ya kifo.

 

Twawezasema kuwa Neno la Mungu limebaki kuwa siri ambayo haijulikani kwa uhakika nao wanadamu wa kizazi hiki. Wengi hulisikia lakini wakiwa na macho na masikio yao yamefumbika, kuashiria nia iliotiwa pazia ili wasiwezepambanukiwa na Kweli ya Ule Ujumbe wausikiao; ni kama kusikia fumbo fulani na ukakosa kupambanua maana na ujumbe walo. Neno la Kweli lake Mungu hufunua Ukweli na Uzima uliomo ndani Yake, ambao ni Uzima uliofichika ndani Mwake Mungu. Hilo Neno hufunua Njia au Milki ya Roho Yake Mungu mahali ambapo giza huyeyuka na kuisha. Milki hii ii hai na sio jambo la kesho au mawinguni mahali Fulani pengine tukifa, kama vile didni na imani ya wanadamu inavyotaka tuamini. Ili kuridhi mahali hapa pa Uzima, na Baraka zisizo kipimo, kile tunachohitaji ni masikio yetu kufunguliwa kimakini ili kusikia, na ndipo tutakapotambua kuwa ulimwengu huu tulio sio dhabiti, mbali ni kiwiliwili kisicho hai. Kama tutakavyotambua,  Henoko aliwezaepuka kusyagwa na kifo kwa sababu alivumbua hii siri ya Uzima; Aliweza kusikia na kupokea kutoka kwayo Sauti Ya Roho. Na ndio maana Yesu akadhibitisha kwa uhakika kuwa, tazama unavyosikia;

 

Marko 4:24-25.

24 Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.

25 Kwa maana mwenye kitu atapewa, naye asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.

 

Tukipokea kwa unyenyekevu Mbegu isiyoharibika ya Neno la Roho, tutajitwalia lote lililo la Mungu na twajua kweli kuwa yote ni Yake; lakini mwanadamu asipopokea kutoka kwa Roho, yeye humalizia na kuzikwa pamoja na vitu vilivyokufa na pale yeye hupoteza kila kitu hata kile alichofikiria ako nacho, na hataiona ile milki ya utukufu yake Mungu ambayo imehifadhiwa wale walipendalo Jina Lake Bwana. Kuna Mahali ambapo giza huisha. Twawezapaita Ufalme wa Mungu au Paradiso yake Mungu ama Mbinguni au Mlimani Sayuni. Ni milki iliyoko, kwa kuwa imekuweko, hata kabla vionekanavyo kuwahitokeza. Moyoni mwake mwanadamu kunaye shahidi ya Milki hii isyo na uharibifu. Na ndio maana kupitia fikra na mawazo ya kiwanadamu, ambayo ndio mwamba wa dini, tafakari za migawanyiko ya tamaduni na imani za kiwanadamu, yeye hujaribu asiweze kufikia Kilele kile. Tusidanganyike ndugu zangu. Dini, iwe kikristo ama nyingine yeyote, haziwezitambua Paradiso yake Mungu. Ni kama aliyepofuka akimwongoza kipofu mwenzake. Na twajua kwa uhakika kuwa wote wawili hutumbukia shimoni. Damu na nyama, amabazo zaashiria mawazo ya kiwanadamu na kuelewa (au kutoelewa kwao) haviwezikuiona hii Milki yake Mungu, nusura kuingia.

 

MILKI YA NURU NA UZIMA

Akinena kupitia Roho, Ayubu anashuhudia kuhusu hii Milki isiyo na uharibifu, mahali ambapo mwanadamu humaliza giza, na kuvumbua yale madini ya dhamana yaliyofichika chini ya uvuli ya giza.

Ayubu 28:1-11.

1 Hakika kuna shimo wachimbako fedha, Na mahali wapatapo dhahabu waisafishayo.

2 Chuma hufukuliwa katika ardhi, Na shaba huyeyushwa katika mawe.

3 BINADAMU HUKOMESHA GIZA; HUYATAFUTATAFUTA HATA MPAKA ULIO MBALI, MAWE YA GIZA KUU, GIZA TUPU.

4 Hufukua shimo mbali na makao ya watu; Husahauliwa na nyayo zipitazo; huning’inia mbali na watu; huyumba-yumba huko na huko.

5 KATIKA ARDHI NDIMO KITOKEAMO CHAKULA; Na chini yake hupinduliwa kama kwa moto.

6 MAWE YAKE NI MAHALI ZIPATIKANAPO YAKUTI; Nayo ina MCHANGA WA DHAHABU.

7 NJIA ILE HAPANA NDEGE MKALI AIJUAYE; WALA JICHO LA TAI HALIJAIONA.

8 WANYAMA WAKALI WAJIVUNAO HAWAJAWAHIKANYANGA; WALA SIMBA MKALI HAJAIPATA.

9 Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake; Huipindua milima hata misingi yake.

10 Hukata mifereji kati ya majabali; NA JICHO LAKE HUONA KILA KITU CHA DHAMANA.

11 Hufunga vijito visichuruzike; NA KITU KILICHOSITIRIKA HUKIFUNUA.

Ayubu 28 ni fumbo la mchimba migodi anayechimba chini mwa ardhi, na kuingia mahali pa giza  ambapo wanadamu wengine hawajui, na hupata hazina ya migodi ya dhamana. Hii inalingana na ule mfano Yesu alipatiana kuhusu hazina ya dhamana iliyofichwa ardhini (Mathayo 13:44). Hiyo hazina ya dhamana ni kiashirio mwafaka cha utukufu wake Mungu ulioficchwa ndani ya Mwanadamu, na ndio unaoitwa mahala pengine Kristo-Ndani-Yako-Tumaaini-La-Utukufu. Pamoja naye Kristo huyo ufalme wa Mungu na utimilifu wa kile Mungu Alicho na Alicho nacho.

 

Upumbavu wa moyo wa mwanadamu wa jinsia ndicho kinachotunga kifo, na ndicho kinachoficha Uttukufu wake Mungu ndani mwake. Hii nddio ile ile giza ambayo imefunika uso wa vilindi vya maji katika Mwanzo 1:2. Mwanadamu huondoka na kuellekea maishani akiwa na hisia za dhambi na ufukara na huendelea kuzama katika masumbuko naa uharibifu na maangamizi kwa sababu ya ujinga uliomo ndani  ya moyo wake. Hajui kule alikotoka, na haelewi kabisa kule anakoelekea. Hajui kwa uhakika kile alichoumbika kwacho. Lakini ssasa, kwa furaha na shukrani tunatangaza kuwa Nuru inaangaza. Na ile njia ya Kiungu ya Uzima wa milele iladhihirika kila kuchao. Na tumeanza kuona kile ambacho ndege na samba wakali walikosa kuona na kusema, kasoro kutembelea. Tai na simba ni ishara ya vile vitiavyo najisi, ambavyo ni vya kinyamaa na damu (yani mwanadamu wa kijinsia), ambaye twaajua haawezikuuingia Ufalme wa Mungu. Mwanadamu anapobaki katika hali yake ya kinyama na damu, hawezi kuiona ile Milki ambayo imejaa mchanga wa dhahabu, yakuti na mkate (ambayo ndiyo lile jiwe amethisto au mana). Hii ndiyo picha halisi ya Paradiso yake Mungu (Mwanzo 2:8-12), Milki ya utimilifu, Nuru kamili, na furaha ambayo hamna kitu kinachotia najisi, wala kitiacho uongo huingia. Mchanga wa dhahabu waonyesha Uungu na hali ya kutokufa, hai ya umilele; na yale mawe ya yakuti yaashiria usafi na utajiri wa utukufu; ilhali mkate (mana au jiwe la amethisto)) yaashiriia Uzima wa Kiroho uliojaza mahali pale pa Uhai wake Mungu.  

 

Hii ndio Milki ambayo Henoko alivumbua na ndio ile ile Milki ambayo kila mmoja wetu atakusanywa na kutwaliwa kwake, ndio tukaweze kuishi kwenye ile Nuru isiyosogelewa, ambapo ni Mwana wa Mungu pekee huishi (1 Timotheo 6:16). Hakuna awaye yeyote anawezaingia mahali pale pa Uzima, kwa sababu akili na hisia zake mwanadamu zimetiwa giza kwa ajili ya kinachonajisi katika Ulimwengu huu tulio. Ni wale tu waliokombolewa kwake Mungu kupitia Kristo, wale ambao wamefuata mwongozo wake Roho wa Mungu hata kufa kwao katika maisha walioishi katika ubatilifu wa ulimwengu ulioko ambao wataweza kuingia mahali hapa pa Uzima.

 

Miaka mingi baada ya Ayubu kuondoka duniani, Roho wa Bwana anadhibitisha Milki hii ambamo kifo huisha ipo;

Isaia 35:8-10.

8 Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia Ya Utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao wasafirio; wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.

9 Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo.

10 Na hao waliokombolewa na BWANA watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.

 

Watakaopata mahali hapa hawataonja kifo tena.  Hawa ndio wale ambao yesu aliwaita Wana Wa Ufufuo, wale ambao sio wa ulimwengu huu tulio, mbali ni wa ule unaokuja (Marko 9:1). Hawa ni wale ambao katika kizazi hiki waonekana kama wajinga, kwa sababu wanaishi kwa Hekima ya Kiungu, ambayo ni ujinga kwao walio wa dini na walio na fikra za kidunia na za mwanadamu wa ulimwengu huu. Hawa ndio wale waijuao sauti ya Mwalimu wao na wamfuata hata katika kupaa kwake, hata kuingia mahali pale pa pumziko na furaha ya milele. Haya mambo tuyasikiayo ni ile siri yake Mungu iliyofichwa kwao wafalme (wana wa wanadamu) wa kizazi hiki, lakini yamepeanwa kwa yale maskio ambayo yako tayari kumsikia hekima anapowaita watu. Kwa hili, Yesu asema, “Heri ni masikio yenu kwa sababu yanasikia, na heri ni macho yenu kwa sababu yanaona”, kwa sababu kuna umati…wale walio na hekima, wanayatafuta mambo haya lakini wasiyapate.

 

Kwa kuzaliwa katika ulimwengu tulio, na kulewa na roho ya kizazi hiki ambayo baada ya hapo imetuunda kuweza kuishi kupitia husia za kijinsia, wanadamu wametayarishwa na kujengeka ili kutafuta ishara za kijinsia. Kwa hivyo, hawawezielewa Kweli iishiyo ya kiroho ambamo Uzima upo. Kwa kutojua, mwanadamu huufunga mlango huu wa Ufalme wake Mungu kwa uso wake mwenyewe kupitia imani zake and matarajio yasiyoafikiana. Yeye huwa hatizami na kutafakari maneno hakika yake Yesu yasemayo, UFALME WA MUNGU UMO NDANI MWENU. Kumaanisha kuwa, utimilifu wake Mungu umo ndani mwetu na twajua kwa uhakika kuwa ndani mwake Mungu hamna kifo. Haya maneno yake Yesu yanapingana bayana na imani na itikadi za kidini zao wanadamu wa kizazi hiki, amabao imani zao ni kama nyuta zinazowasitiri wasiingie wala kuuona Ufalme wake Mungu.

 

Lakini leo tunawezakiri kwa ujasiri kupitia Roho wake Bwana kuwa kuna hisabu ya watu waliosalia, mabaki yake Bwana amaabao hawatafuata njia panda ambayo inaelekea mautini, lakini kama Henoko, hawa wataipata ile njia nyembamba ielekeayo Uzimani mbali na mateso na uharibifu ulioko mautini kule chini. (Mithali 15:24). Kama tujuavyo, bibiblia hunakili mifano michahe ya watu ambao hawakuonja mauti; Hii mifano imenakiliwa kimakusudi ili ituelimishe katika ile njia ya Uzimani. Mmojapo wa wale ambao hawakuonja mauti alikuwa ni Eliya, aliyesafirishwa hadi mbinguni kwa upepo wa kisulisuli na jeshi la waendeshaji farasi na gari la moto (Tafadhali soma chapisho “GARI NA WAENDESHAJI FARASI WA ISRAELI”). Mtume Paulo anapowaandikia Waebrania, anaponakili kuhusu wakuu wa Imani, anamzungumzia Henoko ambaye alihamishwa naye Mungu ili asije akayaonja mauti kwa sababu ya ushuda wake kuwa alimpendeza Mungu.

 

Waebrania 11:5.

5 Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.

 

KUMKARIBIA MUNGU ILI KUMPOKEA ROHO WAKE

Katika sura ya tano ya kitabu cha Mwanzo, twaona bayana kuwa Henoko aliishi miaka mia tatu yake ya mwisho akitembea kwa ukaribu sana naye Mungu, halafu hakuweko tena, akatoweka. Lakini twajua kuwa Mungu yupo vizazi hata vizazi.

Mwanzo 5:22-24.

22 Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume kwa wake.

23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano.

24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.

 

Ni pale tunapotembea kwa ukaribu na Mungukama Henoko alivyotembea tutakapokuwa na ushindi dhidi ya mauti. Kama vile maji na mafuta hayatangamani, huo Uzima hauna lolote la kuambatana na mauti, kama vile tujuavyo kuwa ndani mwake Baba hamna giza hata chembe. Pia twajua kuwa Mungu kila wakati yu tayari kuwapa kila kitu kilicho Chake kwao wote wanaoitisha, kwa kuwa yeye huwapa wote Nuru; sio tabia yake Mungu kumnyima chochote chema kwake mwanadamu yeyote. Chote chema chaja kutoka kwake Mungu, Baba wa Nuru, na yeyote apokeaye kutoka kwake Baba hutiwa Nuru Ya Uzima, kwa sababu hilo ndilo tu Mungu alilo nalo. Saka na utapata, uliza na utapewa, bisha na mlango utafunguliwa kwako wewe. Swali ni; TULISAKALO NI LIPI? Je, ni utajiri wa kilimwengu, afya njema, familia nzuri, makaazi na kazi, na kutajika mbele za wengine ama twasaka Uzima wa Milele uliofichika ndani mwake Mungu!Lazima tuanze tuanze kubadili mtazamo wetu kuhusu tumaini la mwito tulio nao, ambao sio mwingine ila kupatikana ndani mwake Kristo, Ambaye ni mmoja na Baba Mungu milele, ama kwa msemo mwingine, Yeye aliye Mungu kweli na Uzima wa milele (1 Waraka wa Yohana 5:20). Tukiwa Naye, tunavyo vyote; kwa njia hii Yeye asema, tafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haya yote mtazidishiwa. Nia kamilifu imelengwa kwa utukufu wake Kristo Aliye juu na hii ndio inapaswa kuwa nia ya kila amsakaye Mungu; kilio chetu kwa undani ni kuwa sawia na hii Nia Yake Mungu.

 

Kila mtu aitafutaye njia ielekeayo Uzimani itambidi atembee karibu na Mungu na Roho wake Mungu amwongoze, kwa sababu ni Roho wa Mungu pekee anayeweza kuwaongoza wanadamu kutoka kwenye mauti wanakosaga meno walio ulimwenguni huu. Tumeanza kupata umuhimu wa Roho wake Mungu anayetufunza kutoka vilindi vyake Mungu.

Na tukaangalie kwa umakini maandiko haya yaliyoko Zaburi, yanayoelezea kwa undani nia na fikra za Yule anayemsaka Mungu. Yanaelezea fikra za Yule ambaye atapata mahali pa Uzima wa kweli.

Zaburi 16:7-11.

7 Nitamhimidi BWANA aliyenipa shauri. Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.

8 NIMEWEKA BWANA MBELE YANGU DAIMA, kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.

9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahi. Nao utukufu wangu unashangilia. Naam, mwili wangu nao unakaa kwa kutumaini.

10 MAANA HATAKUACHIA KUZIMU NAFSI YANGU. WALA HUTAMTOA MTAKATIFU WAKO AONE UHARIBIFU.

11 UTANIJULISHA NJIA YA UZIMA; MBELE ZA USO WAKO ZIKO FURAHA TELE; NA KATIKA MKONO WAKO WA KUUME MNA MEMA YA MILELE.

 

Zaburi 73:23-28.

23 Walakini mimi ni pamoja nawe daima. Umenishika mkono wa kuume.

24 UTANIONGOZA KWA SHAURI LAKO, NA BAADAYE UTANIKARIBISHA KWA UTUKUFU.

25 NI NANI NILIYE NAYE MBINGUNI, WALA DUNIANI SINA CHA KUNIPENDEZA ILA WEWE.

26 Mwili wangu na moyo wangu hupunguka. Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu na sehemu yangu milele.

27 MAANA WAJITENGAO NAWE WATAPOTEA; UMEWAANGAMIZA WOTE WALIOKUWACHA WEWE.

28 NAMI KUMKARIBIA MUNGU NI KWEMA KWANGU. Nimefanya kimbilio kwa BWANA MUNGU niyahubiri matendo yako yote.

 

 Zaidi ya yote, anayemsaka Mungu kwa ukweli na kumsongelea Yeye kwa moyo wake wote na nia  yake yote ameweka mawazo yake kwa Mungu pekee; kumaanisha kuwa Mungu pekee ndio kittu chake cha dhamana mbinguni na hata duniani. Hii ndio njia pekee ya kuingia Uzimani (Zaburi 73:25, 16:8).Hii ndio katika Ufalme yaitwa kumsaka Mungu kwa nia moja. Watakaoingia wanafanya vile kwa uamsho wao kuuona Ukweli kuwa Mungu ni yote ndani ya vyote. Mwanadamu akiona vingine, yeye huongozwa na lile jicho lililoovu ambalo maono yake ni sanamu (ubatili) na baadaye humweka katika uharibifu.

 

Wakati Mtume Yohana anaposema, “Watoto wadogo jilindeni nafsi zenu na sanamu” (1 Yohana 5:21) anamaanisha kaeni mbali na kitu chochote ambacho hakimfunui Mungu wa kweli na Uzima wa milele. Jicho lililo ovu ni mtazamo wake mwanadamu unaoangalia yaliyoumbwa kutoka katika mtazamo wa kimwili na kijinsia, bila kutambua kuwa mambo yote katika jinsia yanaashiria mambo yaliyokweli ya Mungu yasiyoonekana kwa macho. Mtume Paulo alijua siri hii na akasema, “Simtambui yeyote tena kwa mwili bali kwa Roho”, kumaanisha kuwa ndani ya kila mwanadamu anatambua Mbegu yake Mungu ambayo ni Kristo. Hii ndio njia pekee ya kuondolewa mawaa na kuwa na Upendo umbao bila, hamna mtu anayeweza kusimama mbele za uwepo wake Mungu.

 

Kwa jicho safi, ndipo palipo na Uzima pekee…Mtu mmoja…Mwili mmoja…Roho moja…Jamii moja…Kanisa moja…Kusanyiko moja…na Mungu mmoja. Mengine yote  ni sanamu ambazo zaisha na kutokomea na wakati. Basi mmoja awezauliza “Nitafanya nini kuhusu jamii yangu niliyo nayo kimwili au washirika wa kanisa ninalloshiriki?” Jibu ni rahisi sana. Waambie Ukweli ili hata wao wakaoolewe na wakauondokee uharibifu wa mauti iliyo chini.

 

Ili kupokea Nia hii iliyo juu kuliko ilivyo ndani yake mwanadamu, lazima tujengeke kikamilifu kupitia Roho wake Mungu, kwa kuwa wale watakaoingia katika Utukufu ni lazima wafunzwe  na kufunzika kwake Mungu  (Isaya 54:13). Ushindi wake Henoko juu ya kifo uliwezekana kwa sababu yeye aliposogea kwake Mungu na kumfanya Mungu mahali pake pa siri, aliongozwa moja kwa moja naye Mungu. Mwongozo huo aliopewa naye Mungu ni mwongozo unaowapotea wengi katika kizazi hiki. Ni huu mwongozo kupitia Roho wake Mungu ambao humuinua mwanadamu  kutoka vilindi vya mauti na kumweka tena kwenye mkono wa kuume wake Mungu mahali ambapo ataona tena furaha, amani, na Uzima wa milele. Kifo hakina milki yeyote ndani ya watakatifu waake Mungu. Ni kwa sababu wale wanaoungamanika na kuwa mmoja naye Roho wa Mungu wanapokea mwongozo kutoka kwa Mungu pekee (1 Wakorintho 6:17).

 

Katika uasi tulishushwa na kuwa viumbe wa mavumbi tu. Lakini kupitia Roho Ambaye ni Pumzi kutoka vilindi vyake Mungu, twarejeshwa katika mbingu tuliposhuka kutoka ndani yake Mungu. Roho ndio tu karama yake Mungu kwa mwanadamu, ambayo bila hiyo hakuna mtu yeyote anawezaepuka nguvu za kifo na mauti ambazo zatawala ulimwengu tulio sasa (Matendo ya mitume 1:4)

Tujikusanye tena katika tafakari hii na tujikumbushe kile Yesu na mitume wake walichokisema kuhusu Roho wa Mungu.

 

ROHO ASHUHUDIA KRISTO ALIYE NDANI YETU.

  Yohana 14:16-17.

16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele.

17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

Yohana 15:26-27.

26 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, YEYE ATANISHUHUDIA.

27 NANYI PIA MNASHUHUDIA, KWA KUWA TANGU MWANZO MMEKUWAPO PAMOJA NAMI.

 

Kile Yesu anachosema kwa muhtasari ni kuwa Roho wa Mungu ndani yetu anashuhudia Kristo, Ambaye ndiye Kiumbe cha Kweli kutoka kwa Mungu toka Mwanzo. Wakati Yesu anazungumza kujihusu anaposema, “Yeye Atanishuhudia”, haashirii wala kuzungumzia lile umbo alilolivaa wakati ule miaka 2000 iliyopita…bali anazungumzia Yule Mtu wa ndani wa Roho, aliyefichika ndani ya kila mwanadamu. Huyu mtu wa ndani ni ndiye Kristo…ndiye Mfano wake Mungu…ndiye utukufu wake Mungu. Nuru itokayo kwa Roho wa Mungu ndiyo ituamshayo na kutufanya hai na kutambua kuwa SISI NI KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYEKUWEKO TANGU MWANZO. Hii ndio kweli Takatifu tulioisahau tuliposhushwa katika ulimwengu huu tulio na kufanyika mwanadamu wa mwili na nyama.

 

Kristo ndiye Roho na Yeye hushi kifuani mwake Baba milele. Yeye ni mmoja na Baba, kumaanisha kuwa hana kitu kiitwacho kifo ndani mwake. Roho wake Mungu ndani yetu ashuhudia na kukubaliana na roho zetu kuwa sisi ni wana wa Mungu, tulio huru kutokana na udhaifu uliojenga ulimwengu tulio sasa hivi, na sisi ni waridhi halali wa Ufalme wake Baba wa milele.Huu ndio Ukweli wa kiungu unaotufungua kutoka vifungo tulivyovifikiria vya nguvu za kifo na mauti, kwa kuwa Mwana wa Mungu hafi bali aishi milele (Yohana 8:35)

 

ROHO AFUNUA MILKI HII ILIYOBARAKA KWA WALE WANAOIKUBALI

Yohana 16:13-16.

13 Lakini Yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awtie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.

15 Na yote aliyonayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari. Huzuni itageuka na kuwa furaha.

16 Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni; na tena kitambo kidog nanyi mtaniona.

 

Roho wa bwana atuongoza sis katika kila kweli, akitufunnulia sisi mambo yajayo. Mambo yajayo katika somo hili ni mambo yaliyo katika Ufalme wake Kristo. Haya yatufungua macho kuona mambo ambayo yamefichika kwa muda sasa. Uwepo wake Baba ambao mahali kwingine waitwa Paradiso wawezapatikana na kujulikana sasa. Hamna yeyote anayewezatambua  Milki hii barikiwa ambamo kifo na mauti vyaisha asipoongozwa naye Roho wa Mungu. Roho ndiye atufanyaye tutambue Milki hii ya Utukufu ambayo macho ya mwili ya mwanadamu hayawezi kuona (1 Wakorintho 2:9-13). Wanadamu wa kizazi hiki waendelea tu wakitumbukia huku na kule wakitafuta ishara kwenye ulimwengu wa damu na nyama kuhusu huu Ufalme wa Mungu, bila kujua kuwa UPO MILELE.

 

KAZI IBADILISHAYO YA ROHO ITUFANYAYO SAFI

 Ni dhahiri kwetu sote kuwa bila utakatifu wa kweli na haki yake Mungu ndani mwetu, hakuna awezaye kuona wala kuukaribia uwepo wake Mungu. Dhamiri inajihukumu na nafsi ilipotoka haiwezi kamwe kuingia katika Ufalme wake Mungu. Mungu hamfukuzi yeyote toka Uwepo wake. Ni nafsi na dhamiri yake mwanadamu ambayo humsukuma na kuweka vikwazo katika njia ambayo ingemrudisha kwake Baba. Na twajua kuwa wale wanapotoka kutoka uwepo wake Baba wanatupwa kwenye mashina ya uharibifu na mauti (Zaburi 73:27). Twajua pia kuwa wanadamu wote ni wapotovu na wameweka malazi yao mautini (Psalms 53:1). Swali ni, tutatokaje kule na kupata njia ya kurudi tena kwenye uwepo wake Baba, mahali ambapo tutapatana tena na furaha?

 

Ufunuo 21:27.

27 Na ndani yake hataingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.

 

Ni kupitia tu kwa roho wake Mungu ambapo tunawezatakasika na kubadilishwa kutoka hali ya mauti na ya kumpinga Kristo ambayo tumeiridhi kwa kuzaliwa kwetu na tohara iliyotuambatanisha na ulimwengu huu wa sasa (1 Wakorintho 6:11). Yeyote yule anapochagua kuendelea kuishi kama mwana wa damu na nyama, roho amabayo inatawala kizazi hiki, ni hakika kuwa Yule mtu atafa katika dhambi za uasi wake. Lakini Yule mtu akitubu na kumkubali Roho wa Bwana achukue hatamu za usukani, basi Yule mtu atafunguliwa kutoka kifungo cha dhambi ya uasi. Roho wa Mungu atampa hali ya kiungu, lakini nafsi ya mwanadamu inatunga kiumbe ambacho hakiwezisadiki kwake Mungu.

 

KUINULIWA KWETU NA KUKUSANYIKA KWETU KATIKA UTUKUFU WAKE MUNGU

 

Roho Yule Yule (ambaye ni Roho wake Mungu) Aliyemwamsha Yesu toka kwa wafu na kumketisha mkono waa kuume wake Mungu yu kazini katika kila mtakatifu ili kumfufua yeye na kumwinua juu ya nguvu zote za kifo na mauti. Yatie akilini kuwa kifo cha kweli ni hali ya kiroho, wala sio kuuwacha mwili huu tu. Ni kutengwa naye Mungu, ambaye ndiye chanzo cha Uhai na Uzima. Tukiishi kama wanadamu tu waongozwao na hisia za kinyama kama walivyo wanyama mwitu, hatutawezahisi Upendo wa Milele utokao katika uwepo wake Baba. Tutakuwa tumekufa katika dhambi zetu na uasi na kuvuna ndani mwetu mshahara wa kifo na mauti. Hofu, hali ya kukosa na madhara mengine mengi ambayo wanadamu hupitia ni ishara dhabiti kuwa kuna matunda au mshahara wa kifo na mauti. Anayewezakana kuwa hajapitia yale ndani mwake hana kweli ndani mwake. Lakini tukikiri uasi wetu katika adamu na kuikubali Sauti ya Kweli,Yeye ni mwaminifu wa kutusamehe.

 

Tunda hatima la msamaha wake Mungu kwetu ni sisi kujitambua tena kama Mmoja katika Kristo, jinsi tulivyokuwa kabla ya kushuka katika milki hii (ulimwengu) iliyotengeka toka kwake Mungu. Tutaweza tena tawala na kupata pumziko katika Uttukufu wake Baba. Alipo Yeye (Mwana wa Mungu), ambapo ni mkono wa kuume wake Mungu, papo hapo ndipo waliokombolewa wake Mungu watakapokuwa (, papo hapo ndipo waliokombolewa wake Mungu watakapokuwa (ohana 17:24). Mahala pale ndipo tutakapojua utele wa Uzima, Haki, Usafi na utulivu kamili bila hofu yoyote ile. Wanaoshiriki wokovu wa kweli ni wale wanaoupata ule mlima Sayuni, mahali pa mchanga wa dhahabu n mana tele tele, na wao husimama kama Mmoja na Aishie; kama Henoko, hawataonja kifo.

 

Marko 9:1.

1 Akawaambia, amin nawaambia, pana watu katika hawa wasimamao hapa, amabao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona Ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.

 

Hawa ni wale wautambuao Ukweli na pale wanachukia hata maisha yao katika ulimwengu huu ili waungamanike kuwa mmoja katika ule Uzima wake Mungu Mtakatifu. Kuutambua Ukweli na kuishi katika ule Ukweli, Baba huwaheshimu na kuwatukuza na Nafsi Yake Yeye Mwenyewe, ili wao waweze kuridhi pamoja katika utukufu wa kiungu na Uzima wake Mungu.

 

Yohana 12:25-26.

25 Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata Uzima wa milele.

26 Mtu akinitumikia, na anifuate, name nilipo ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu. Yesu alinena kuhusu kifo chake.

 

Cha kutisha ni kuwa Henoko alitabiri kuhusu kuweko kwa hili kundi la waliokombolewa ambao wanakusanywa katika mahali pa Uzima kumtumikia Bwana.

 

Yuda 14, 15.

14 Na Henoko, mtu was aba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu, maelfu.

15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.

 

Hili kusanyiko la maelfu ya watakatifu lajulikana kama Kanisa, Malaika au Wana wa ufufuo ni wale waliokamilika ambao hata sasa wankusanywa mlimani Sayuni na wanatokea ulimwenguni katika utukufu kamili wake Baba. Yesu pia aliujulisha ulimwengu kuhusu hawa ambao wamekombolewa watakaouhukumu ulimwengu na kuusawishi kuhusu dhambi zake (Marko 8:38). Kufunuliwa kwao kwenyewe kwaleta hukumu ulimwenguni kuhusu dhambi zake na kuwafanya wanadamu kuwaza Mungu asiyeonekana ambaye anadhihirika mwilini kwa sasa. Henoko yuko ndani ya lile kundi la maelfu, mtume Paulo pia na watakatifu wote wa zama zile na hata wa sasa.

 

Yesu ndiye Njia, Kweli na Uzima pekee. Hakuna awezayee yeyote kuuona wala kuuonja Uzima huu wa kiungu ila kwa kupitia kwake Mwana Aliye Mmoja milele na Baba. Hii yaelekeza kujielewa kwetu katika Kristo na kupotea kabisa kwa ufahamu wetu kuwa sisi ni wanadamu tu ambako tulipokea tuliposhuka ulimwenguni huu. Kwa upumbavu na makosa, mwanadamu amufumwa kuishi kulingana na mambo yaliyo nje, kulingana na mtazamo wake wa mambo yaliyo duniani. Na anapoendelea kuishi hivi, yeye ataishi tu kama mwanadamu na kufa.Lakini akihisi Roho wake Bwana akimwita, na kutubu, kwa kujiambatanisha na hali yake ya mbele ambayo ni Kristo, ambaye ndiye Kiumbe Halisi chake Mungu, basi yeye huyu mwanadamu atapita kutoka kifo kurudi Uzimani na zaidi ya pale kujua furaha ya milele.

 

Ayubu 36:8-12.

8 nao wakifungwa kwa pingu wakitwaliwa kwa kamba za mateso;

9 Ndipo huwaonyesha matendo yao, na makosa yao, ya  kuwa wametenda kwa kujivuna.

10 Yeye huyafunua masikio yao, wasikie maonyo, na kuwaagiza warudi kuuacha uovu.

11 Kama wakisikia na kumtumikia, watapisha siku zao katika kufanikiwa, na miaka yao katika furaha.

12 Lakini wasiposikia, wataangamia kwa upanga, nao watakufa pasipo maarifa.

 

KUTWAALIWA KWAKE HENOKO KATIKA UTUKUFU WAKE MUNGU

 

Imenakiliwa kuwa Henoko alimpendeza Mungu. Kwa hili pekee, Mungu alimvuta hata akatoka katika vilindi vya kifo na mauti. Mtu awezauliza, “Lipi hili linalompendeza Mungu?”  Lile tu linalompendeza Mungu ni ubatizo wetu katika kifo chake Yesu katika mwili, na kuambatanishwa na Kristo Roho Ambaye Ndiye Mwana wa Mungu. Mungu adhihirisha hili katika ubatizo wake Yesu alipoguruma toka mbinguni na kusema; “Huyu ndiye Mwanangu Pekee anipendezaye…” (Marko 1:9-11). Hii sauti ilikuja tu baada ya ubatizo wake Yesu. Inamaanisha kuwa maisha Yesu aliyoyaishi wakati ule hayakuwa ya manufaa. Kutoka wakati ule Yesu alipobatizwa na kujazwa na Roho Mtakatifu, ni Nafsi Mpya iliyoishi na kutenda kazi kuanzia pale. Ni Mwana wa Mungu Aliyekuwa tangu Mwanzo, sio Myahudi Fulani aliyezaliwa katika hori la ngombe mahali fulani miaka thelathini hapo mbele.

 

Mwili na damu haviwezikiri kama Yesu kuwa “Mimi hufanya daima mambo yampendezayo Yeye…” Hii ni kwa sababu haviwezi kuambatanishwa na mapenzi yake Mungu. Kama Paulo anavyoandika katika nyaraka zake, Roho na mwili havisikilizani wala kuambatana. Inamaanisha lazima tukome kujaribu kuufanya mwili ukubalike mbele za Mungu. Itatubidi kufikia Roho na kwa imani tukaweze kutembea katika ufunuo wa nuru ya Roho. Ili kuridhi Uzima wa milele, itatubidi kuachilia nafsi zetu katika huu ulimwengu tuishio na tushikie Uzima wetu wa kweli katika Roho. Tukippanda katika Roho kwa uvumilivu, tutapotelea kifo; lakinitukishikilia kilicho ongo (mwili) au nafsi yetu ya kiwanadamu, tutazikika pamoja na wengi wanaomalizia mautini. Kama tujuavyo, Mungu haleti maangamizi na mauti kwa yeyote. Mwanadamu hujiletea yale juu yake yeye mwenyewe kwa kutosikia mashauri yamfaayo.

 

Wagalatia 6:7,8.

7Msidanganyike, mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

8 maan yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna Uzima wa milele.

 

Siri ya kuhamishwa kwake Henoko ni kuwa aliacha kuwa kiwiliwili kilichotengeka na Mungu wake. Nafsi yake katika mwili ilimezwa katika moto wa Upendo wake Mungu, na Mungu akawa yote ndani ya yote. Hii ni ishara kuhusu mwisho wa imani yetu…wakati ambapo Kristo ataweka kila kitu chini ya miguu Yake na mwishowe atu kabidhi kwake baba Ambaye atakuwa Yote Ndani ya Vyote. Katika hili, kila kuelewa na maarifa kwaisha. Mataifa yote yafanyika Moja Ndani Ya Bwana.

 

1 Wakorintho 15:24-28.

24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba Ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.

25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.

26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.

27 Kwa kuwa alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.

28 BASI, VITU VYOTE VIKIISHA KUTIISHWA CHINI YAKE, NDIPO MWANA MWENYEWE NAYE ATATIISHWA CHINI YAKE YEYE ALIYEMTIISHIA VITU VYOTE, ILI KWAMBA MUNGU AWE YOTE KATIKKA WOTE.

 

Roho wa Kristo ni kama moto ulao ndani yetu unaoangamiza kila ngome na utawala ndani yetu ambao unajaribukujikweza dhidi ya maarifa ya Kristo. Na hizi ni zile imani za wanadamu zinazotufunganisha na maisha haya ya mwili na damu na uhai uliotengeka na Mungu. Hizi imani duni ndizo zile zilizomtunga mtu wa dhambi ambaye hawezi kamwe sadiki na kunyenyekea chini ya Mungu. Kazi ya Roho wa mungu ndani mwetu yaangamiza uharibifu huuna Yule mtu wa dhambi ambaye ni mavumbi  na kufunua  mtu wa mbingu wake Mungu ambaye tangu Mwanzo amekuwa ndani yake Mungu. Katika mifano yake mingi, Yesu anaashiria hili kwama makombo yaliyowashwa  moto ili kilicho cha kweli ndani yake (mbegu yake Mungu) ikadhihirike na kukusanyika tena kwenye gala (Mungu mwenyewe).

 

Wengi kule nje bado wamtafuta Yesu Mnazareti kwa mwili kama wale manabii waliokuwa wanautafuta mwili wake Eliya baada yake kutwaaliwa na kupelekwa Utukufuni. Na pengine kama vile walivyoitafuta miili yao Henoko na Musa, lakini wamekosea. Yesu Mnazareti kama mwanadamu Mhebrania hayupo tena, lakini aishi Utukufuni wake Baba kama vile alivyokuwa kabla yake kuja kwake kama mtu wa mwili na damu. Sasa twaelewa kwa nini akasema Yesu kuwa “Narudi kwa Baba”. (Yohana 16:16), ama aliposema, “Baba Nitukuze Tena Na utukufu Niliokuwa nao Kabla Ya Kuumbwa Kwa Ulimwengu” (Yohana 17:5) ama aliposema, “Najua Nilikotoka Na Najua Niendako” (Yohana 8:14). Ubinadamu wake Yesu ulimezwa kabisa na Utukufu wake Mungu; na hiyo ndiyo Mungu alitaka kudhihirisha wakati Yesu alipoinuliwa katika utukufu wake Mungu katika lile wingu, wakati huduma yake hapa duniani ilipokuwa inaisha. Hii ndio ile ile njia kwa wale waisikiao sauti yake Roho ikiwaita kutii ndani ya Yesu, Yeye (Roho Mwenyewe) lazima aongezeke ndani yetu na sisi (mwili na damu) tupungue. Hii ndio njia pekee ya Uzima.

 

Ndugu zangu, wakati ndio huu, sio kesho ambapo ishara za nje zinatimilizwa. Kwa imani twapaswa kuanza safari ya kukwea na kupaa kuingia katika utukufu wake Baba kama Yesu alivyofanya. Hii yamaanisha kunyenyekea kabisa kwake Roho na kubadilishwa kikamilifu kama mashahidi, ili kwamba Baba afanyike yote ndani ya vyote maishani mwetu. Henoko akapita mauti. Zaidi vipi sisi ambao wanatembea katika utimilifu wa neema isiyo kipimo ndani yake Yesu Kristo! Kwake Mungu mambo yote yawezekana na tuna uhuru wa kuingia Uweponi mwake kupitia damu ya Mwana Kondoo, ili yote yawezekane kwetu sisi tunaoamini hii Injili. Kusikia na kuamini hii Injili au Habari Njema inayodhihirisha kuwa sisi ni Kristo katika Utukufu na Mfano wa Mungu aishie ndio cheti chetu cha usafiri kuingia Uzimani wa milele. Kwa hiyo na tuwe na kauli imara ya kupata haya maarifa, na tusikwazike wala kufa moyo wakati majaribu yanapokuja. Tutilie akilini kuwa tunaye Kuhani mkuu ambaye anaelewa udhaifu na unyonge wetu binafsi, kwani yeye mwenyewe aliyapitia haya haya na majaribu ya kimwili.

 

Usiache maneno haya yakutie hofu; tunayasikia maneno ambayo kwa muda yalikuwa yamefichika tusiyajue kupitia kushushwa kwetu kuingia kwenye giza kuu ambalo limeuumba huu ulimwengu. Lazima tuyajue mambo haya ili tuweze kuingia tena katika Nuru na kufurahia utimilifu wa Uzima tena. Kwa furaha na shukrani, twamshukuru Mungu kwa ufunuo wa Ukweli kuhusu uridhi wetu ndani yake.

 

Amina.

Trevor Eghagha.